21 Jan 2016
KIMENUKA!!! WAZIRI WA ELIMU AFUTA MFUMO WA GPA KWA SHULE ZA SEKONDARI NA KURUDISHA MFUMO WA DIVISION, HABARI KAMILI HAPA.
Profesa Joyce Ndalichako akionesha moja ya majibu ya wanafunzi yaliyo jazwa kwenye mtihani wa Taifa(picha kutoka maktaba).
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amefuta mfumo wa uwekaji wa matokeo wa Grade Point Average (GPA) ulioanza kutumiwa na Baraza la Mitihani Tanzania ( NECTA) mwaka 2014.
Mfumo huo uliofuta ule uliokuwepo wa Divisheni na kuanza kutumika kwa kidato cha Nne na Sita,uliletwa kwa kile kinachoelezwa kujaribu kupandisha ufaulu baada ya kuonekana wanafunzi wengi wamefeli mtihani wa kidato cha nne, hasa mwaka 2013.
Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini Dodoma,Waziri Pfrof. Ndalichako ambaye aliwahi kuwa Katibu Mtendaji wa NECTA,alisema Baraza hilo limeshindwa kueleza sababu za kutumia mfumo huo, badala yake limeishia kutoa utaratibu uliotumika tu.
“Kwa mamlaka niliyo nayo chini ya kifungu cha 20 cha sheria ya Baraza la Mitihani Tanzania, sura ya 107, naliagiza Baraza kufanya mapitio ya mfumo unaotumika sasa wa wastani wa alama (GPA) kwa lengo la kurudi kwenye mfumo wa awali wa Divisheni.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako
“Aidha, viwango vya ufaulu vizingatie azma ya nchi ya kuelekea kwenye uchumi wa kati na Tanzania ya Viwanda” Alisema Profesa Ndalichako
Kuhusu mtihani wa pili(paper two), ameitaka NECTA kuufuta kwa watahiniwa wa kujitegemea ambao umeanzishwa kama alama ya maendeleo wakati ni mtihani wa mwisho.
“Wizara haiwezi kufikia azma ya kusimamia ubora wa elimu katika ngazi zote bila kuhakikisha viwango vya ufaulu vinawezesha kutoa wataalam wenye stadi na maarifa badala ya kuwa na wahitimu wengi wenye vyeti, lakini hawakidhi mahitaji ya soko la ajira,” alisema Profesa Ndalichako
Januari 7 mwaka huu, Waziri Ndalichako alitembelea NECTA na kuwataka watoe ufafanuzi wa kuacha kutumia mfumo wa Divisheni na kutumia GPA. Pia aliwataka watoe maelezo ya kuanzishwa kwa mtihani wa pili kwa watahiniwa wa kujitegemea.
Hata hivyo alieleza kuwa maelezo waliyoyatoa NECTA yalijikita katika kueleza utaratibu badala ya sababu za kuutumia mfumo huo.
Source; Global publishers.
0 comments:
Post a Comment