26 Jan 2016

SOMA HAPA NA VIDEO, A TO Z JUU YA MSICHANA ALIYE KUTWA NDANI YA SHIMO LA FUTI KUMI ANAEZANIWA KUWA MSUKULE.

Mwanamke huyo anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 27, aliwashangaza wakazi wa eneo hilo kwani ndani ya  shimo alilokutwa alionekana mchafu, aliyenyongea, akiwa hoi kwa njaa na mtupu kiasi cha kudhaniwa ni msukule (mtu aliyechukuliwa ndondocha).

Ilikuwa Jumanne ya Januari 19, mwaka huu katika shimo hilo lililojengwa na Mtei, inasemekana kuwa, shimo hilo  ni kwa ajili ya chemba ya choo lakini haijaanza kutumika kwa vile nyumba hiyo nayo haijaanza kukaliwa rasmi na familia zaidi ya kuwepo kwa mlinzi.

MAJIRANI WASHANGAZWA
Baadhi ya majirani wa eneo hilo walionesha kushangazwa na tukio hilo huku wakiwa na maswali kuhusu mwanamke huyo ambaye walisema si mkazi wa maeneo hayo na wala hawajawahi kumuona.
maswali hayo ni kama vile;

1. Ni nani aliyemuingiza shimoni mwanamke huyo na kwa madhumuni gani? Kwani kwa jinsi shimo lilivyo, lazima aliingizwa au aliingia kwa kutumia ngazi.

2. Alikuwa akiishi kwa kula chakula gani kwani wakati anatolewa, muda mwingi alikuwa akilalamikia njaa.

3. Swali la tatu ambalo majirani walikuwa nalo, mwanamke huyo aliishi ndani ya shimo hilo kwa siku ngapi? Kwani nywele na kucha zake ziliashiria si zaidi ya mwezi mmoja. Swali kuu, aliingia/ aliingizwa lini na muda gani kati ya mchana na usiku?

4. Je, aliingizwa kwenye shimo hilo akiwa na nguo zake halafu aliyemwingiza/ waliyomwingiza walizipeleka wapi?

5. Swali la tano ambalo majirani hao walikuwa wakilijadili sana ni, je! Mwanamke huyo ni mgonjwa wa akili au ni msukule? Kama si chochote kati ya hayo mawili, kwa nini alikuwa hapigi kelele?

6. Sita, majirani hao waliulizana kama siku za karibuni wamewahi kusikia kwenye vyombo vya habari kuna mwanamke mwenye umri huo anatafutwa? Wote walisema hawajasikia.

7. Wengi walisema huenda mwanamke huyo aliingizwa kwenye shimo hilo na ‘maadui’ wa biashara wa Mtei. Lakini kama ni kweli, walikuwa na lengo gani na walimpata wapi mwanamke huyo na akiwa katika hali gani?

8. Katika mahojiano na majirani wakati bado akiwa ndani ya shimo amekaa, mwanamke huyo aliweza kujibu maswali karibu yote, lakini swali la anaitwa nani na ameolewa au la, yalimshinda kujibu. Ni kwa nini?

9. Polisi Mbezi wanasema wamekuwa wakimpigia simu Mtei, lakini hapokei. Ni kwa nini?

Msukule-(2)
Mwanamke huyo baada ya kutoka ndani ya shimo

MFANYAKAZI WA MTEI SASA
Naye mfanyakazi anayeitunza nyumba hiyo, Richard Pascal alipozungumza na alikuwa na haya:
 “Ninachokumbuka mimi, Jumanne, wiki iliyopita, saa 3:00 asubuhi, bosi wangu Mtei alikuja. Ni kawaida yake kuja na kukagua mji wake.

“Nikiwa naendelea na shughuli zangu, aliniita hapa nje. Nilipofika  aliniambia nichungulie ndani ya shimo. Nilifanya hivyo, nikashtuka sana kumwona mwanamke akiwa mtupu huku akinikodolea macho.
“Niliogopa kwa sababu sikutarajia kama kuna mtu anaishi shimoni bila mimi kujua wakati ndiyo nalinda hapa siku zote.”

AWAITA MAJIRANI
“Niliamua kuwaita majirani. Baada ya muda mfupi watu wakawa wamejazana hapa kila mmoja akishangaa na bosi wangu akatoa taarifa Kituo Kidogo cha Polisi Kibamba ambapo askari walifika.
“Lakini na wao walipatwa na mshangao huku wakijiuliza ni vipi mwanamke huyo aliingia shimoni bila kuumia wala kuvunjika?”

POLISI WAMUHOJI
“Mwanamke huyo alipohojiwa na polisi alisema ameishi humo miaka mingi na mara nyingi alipokuwa akihojiwa alikuwa akililia chakula. Polisi waliniomba ngazi, wakaitumbukiza shimoni kisha yeye mwenyewe akapanda haraka mpaka nje.”

APELEKWA TUMBI
“Polisi walimchukua na kumpeleka Hospitali ya Tumbi (Kibaha mkoani Pwani) ambako nadhani anapatiwa matibabu.”

MLINZI APATA WASIWASI
“Mpaka sasa hivi mimi napatwa na wasiwasi. Nitamuomba bosi wangu aniongezee mtu mwingine ili tuwe wawili, kwani mimi hapa ni mgeni. Nimekuja hapa, Desemba 9, mwaka jana.”

SIKILIZA MAHOJIANO KATI YA POLISI NA MWANAMKE
Polisi: “We, unaitwa nani?”
Mwanamke: (kimya).
Polisi: “Unakaa wapi?”
Mwanamke: “Mbezi Makabe.”
Polisi: “Umeolewa?”
Mwanamke: (kimya).
Polisi: “Umekuja lini hapo?”
Mwanamke: “Hapa kwangu.”
Polisi: Umekuja lini?”
Mwanamke: “Mi njaa inaniuma bwana.”

KAMANDA WA POLISI KINONDONI
Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, ACP Christopher Fuime alipoulizwa kuhusu tukio hilo,  alikiri kulitambua na kwamba, bado wanalifanyia uchunguzi.

Video hii hikionesha namna tukio lilivyokua siku hiyo jionee mwenyewe...


Source: Global Publisher

0 comments:

Post a Comment