20 Dec 2015

ZIFAHAMU CHANGAMOTO KUBWA TANO ZINAZO WAKABILI VIJANA NA NAMNA YA KUKABILIANA NAZO.


Neno changamoto linaweza kuwa na maana kadhaa, katika somo hili, nimefafanua changamoto kama ushindani au mashindano baina ya pande mbili au zaidi, kila upande ukidai uhalali wa kile unachokiamini na hivyo kushawishi upande wa pili ukubaliane na kukifuata kile unachokiamini. Kutoka kwenye dhana ya vita vya kiroho (Waefeso 6:10), Shetani kama mfalme wa giza ndiye mwenye kuzileta changamoto mbalimbali dhidi ya wana wa Mungu kwa nia ya kuwaondoa kwenye nafasi zao za ki-Mungu na hivyo kuwatumia kufanikisha makusudi yake ya ufalme wa giza na mwishowe kuwaharibu kabisa.
Zifuatazo ni sehemu ya changamoto kubwa zenye kuwakabili vijana na namna kijana unaweza kukabiliana na changamoto hizo;

MASOMO NA MAHUSIANO  
Vijana wengi wapo katika rika ambalo wanahaja ya kuoa au kuolewa na wengine bado wanasoma katika ngazi mbalimbali. Katika nyakati za sasa imeakuwa ni changamoto kubwa sana kwa kijana kumpata mwenza sahii wa maisha sambamba na kujua nini asome ambacho kina uhusiano mkubwa na wito wa kusudi la Mungu katika maisha yake.
Tambua kwamba;
 (a) Mungu anapokupa fursa ya kusoma, si suala la kusoma bali kusoma kitu ambacho kipo connected        na future ambayo Mungu amakuandalia
 (b) Si kila mwanamume/mwanamke anafaa kuwa mwenza wako wa maisha. Naam ile kwamba wako       wengi ambao wangetamani kuishi na wewe kama mke au mume ni ishara kwamba wengi wao si         wenza sahihi wa kuishi na wewe. Katika kutafuta na kupata mwenza wa maisha vijana wengi leo       wanatumia akili zao bila kumshirikisha Mungu ipasavyo, wasijue kwamba ndoa isiyounganishwa       na Mungu, ni kikwazo kikubwa katika maisha na kulitumikia shauri la BWANA Mungu wao.


MATUMIZI YA TEKNOLOJIA (MITANDAO)
Kijana mwenzetu Danieli (katika biblia) alionyeshwa kwamba katika siku za mwisho maarifa yataongezeka sana, jambo ambalo ni dhahiri katika kizazi chetu bila shaka. Sote tu mashahidi juu ya namna vijana wanavyotumikishwa na nguvu ya matumizi mabaya ya mitandao mbalimbali ya kijamii. Sote tunaona namna vijana wengi wanavyotumia muda mwingi kusoma na kuangalia vitu visivyofaa kwenye mtandao na mbaya zaidi tunaona ni kawaida. Kadri kijana anavyaongalia vitu vichafu ndivyo anavyoyachochea nguvu ya dhambi na kutenda mabaya ndani yake, naam ndivyo anavyoingiza roho chafu za kila namna ndani yake, hivyo ni lazima kijana kuhepukana na swala zima la matumizi mabaya ya mitandao hasa ya kijamii(imo, facebook, tweeter, whatsapp na mingine mingi)


MAISHA NA UCHUMI
Hali ngumu ya kiuchumi inaleta ushawishi kwa vijana kujiingiza kwenye mambo ambayo si sahii katika jamii na pia yanayo haribu mahusiano yake na Mungu. Naam wapo ambao imefika mahala wameamua kuingia kwenye biashara haramu za madawa ya kulevya, zinaa, uasherati, kutamani kuishi maisha ya kuiga, na mbaya zaidi hata wale ambao wanakiri kumpokea Yesu nao wanaishi maisha ambayo hayana ushuhuda makazini mwao, mtaani mwao n.k hususani linapokuja suala zima la uaminifu, mahusiano na fedha. Ni vyema kijana kujituma na kuwa mbunifu hasa kwenye swala zima la ujasilia mali ikihusisha kutokudharau mtaji ulionao unaoanza nao pamoja na kile ulicho kibuni kama biashara yako na pia kuepuka roho ya uvivu na kusubili kutafutiwa na kutengewa.


KUIPENDA DUNIA
Marejeo:Katika Biblia (1Yohana 2:15 -16).
Ule mstari wa 15 unasema ‘Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia, Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake’. Sisi sote leo tu mashahidi juu ya namna ambavyo vijana wengi, wanavyovutwa na nguvu ya dhambi inayotenda kazi duniani kupitia taama ya mwili, tamaa ya macho na kiburi cha uzima. Shetani kwa kutumia mambo hayo amewafanya wengi sana kuipenda na kuifuatisha namna ya dunia hii, wasijue kwamba nia ya mwili ni mauti na wale waufutao mwili hawawezi kumpendeza Mungu (Warumi 8:5-6).

Pengine zipo changamoto nyingine, lakini hizi tano nilizoziandika ndizo ambazo nimeona umuhimu wake zaidi kuzifundisha kwa kuwa zina athari kubwa sana si tu kwa vijana wenyewe bali zaidi kwenye ufalme wa Mungu.

Imeandaliwa na Mr Patrick Sanga.


0 comments:

Post a Comment