18 Sept 2015

THE HIGHEST TOWER ALL OVER EAST AND MIDDLE AFRICA (Jengo refu zaid Afrika Mashariki na Kati)

Jengo refu zaidi Afrika Mashariki na Kati ni jengo linalo patikana Tanzania katika mji wa Dar es salaam,

Jengo hilo linalofahamika kwa jina la PSPF TOWER ndilo jengo refu zaidi lililo kamilika Afrika mashariki na kati likiwa na urefu wa mita 147, Ukiachilia mbali majengo mengine marefu Afrika kama vile Carlton lililoko Afrika Kusini  lenye urefu wa mita 223, Hassan II Mosque ( mita 219)  lililoko Moroko, Ponte City (173) lililopo Afrika kusini,Necon Hause (mita 160) lililopo Nigeria,Marble Tower(mita 152),Pear Down (mita 152), Met Life Centre (mita 150)na 88 on field (mita 147) yote Afrika ya Kusini.
Jengo hilo lilizinduliwa na raisi Jakaya Kikwete, ujenzi wake ulitumia miaka minne toka 2011 hadi 2015 kwa shilingi bilioni 139.20 za Tanzania lina maeneo ya ofisi na nyumba za makazi 88, Pia katika jengo hilo kuna sehemu ya mgahawa, benki, bwawa la kuogelea, sehemu za zoezi, maegesho ya magari na sehemu nyingine muhimu.


0 comments:

Post a Comment