14 Oct 2015

YAFAHAMU HAPA MAMBO MAKUBWA MUHIMU AMBAYO UJUI KUHUSU MWL JULIUS KAMBARAGE NYERERE, PAMOJA NA PICHA NA VIDEO.


Hayati Baba wa Taifa, Mwl Julius Kambarage Nyerere, enzi za uhai wake.

Historia fupi ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
Jina lake kamili ni Julius Kambarage Nyerere, alizaliwa mnamo tarehe 13 April mwaka 1922 katika kijiji cha Butiama, wilaya ya Musoma, mkoa wa Mara.
Alikuwa mmojawapo kati watoto 26 wa Chifu Nyerere Burito, chifu wa kabila la Wazanaki.
Alipokuwa mtoto Nyerere alichunga mifugo ya baba yake; katika umri wa miaka 12 aliingia shule akitembea kilomita 30 hadi Musoma.
Baada ya kumaliza shule ya msingi aliendelea kusomea shule ya wamisionari Wakatoliki huko Tabora.
Kanisa lilimpeleka chuo cha Makerere, Kampala, Uganda kuanzia mwaka 1943 hadi 1945 kwa minajili ya kuongeza elimu na kusomea ualimu.
Baada ya kumaliza masomo ya ualimu alirudi Tabora akifundisha shule ya St.Mary.
Mwaka 1949 alipata nafasi ya kwenda kusoma kwenye Chuo Kikuu cha Edinburgh, Scotlandi, ambapo alipata shahada ya M.A. ya historia na uchumi .
Aliporejea kutoka masomoni, alifundisha Historia, Kiingereza na Kiswahili katika shule ya St. Francis iliyo karibu na Dar es Salaam. Kazi hiyo ya ualimu ndiyo iliyompatia cheo cha mwalimu ambacho kinatangulizwa kabla ya jina lake.
Alijiuzulu ualimu na kuzunguka nchi nzima ya Tanganyika kuzungumza na watu wa kawaida na machifu ili kuleta umoja katika kupigania uhuru. Pia alizungumza kwa niaba ya TANU katika Trusteeship Council na Fourth Committee ya Umoja wa Mataifa (UN) huko New York.
Uwezo wake wa kuongea na wa kuunganisha watu ulimwezesha kufanikisha Tanganyika kupata uhuru bila umwagaji wa damu.
Kwanza aliongoza Tanganyika toka mwaka 1961 hadi 1964 kama waziri mkuu, halafu kama rais; baada ya muungano wake na Zanzibar, aliongoza Tanzania kuanzia mwaka 1964 hadi mwaka 1985 kama rais.
Mwalimu Nyerere ni kati ya viongozi wachache wa Afrika ambao wameacha madaraka kwa hiari baada ya kutawala kwa muda mrefu, akiwa bado anapendwa na wananchi walio wengi.
Alipostaafu urais mwaka 1985 alirudi kijijini kwake Butiama ambako aliendesha shughuli za kilimo. Hata hivyo aliendelea kuwa na athari kubwa katika siasa ya Tanzania hadi kifo chake tarehe 14 Oktoba 1999 .



Mwl Julius Kambarage Nyerere akiwa na mkewe Bi Maria Nyerere.



Mwalimu Nyerere akihutubia, akielezea kuhusu raisi sahii kwa Tanzania.

Picha mbalimbali za Mwl Julius Kambarage Nyerere,






Familia ya Mwl Nyerere.










Mwl Nyerere akiwa na viongozi mbalimbali wa Afrika.






Mwl Nyerere akimkumbatia raisi Kikwete.






Mwl Nyerere akiwa na Mandela.




Mwl Nyerere akichanganya udongo wa Tanganyika na Zanzibar, ishara ya muungano kuitengeneza Tanzania.







0 comments:

Post a Comment