16 Oct 2015

SIMANZI YATANDA LUDEWA KWA KUMPOTEZA ALIYEKUWA MBUNGE WAO KIPENZI, DEOGRATIAS FILIKUNJOMBE.

Mbunge wa Ludewa Mhe. Deogratias Haule Filikunjombe amefariki dunia katika ajali ya helkopta (Chopa) katika hifadhi ya wanyama ya Selous, pamoja na rubani Kepteni William Silaa mfanyakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa.
Wengine waliofariki kwenye ajali hiyo ni Vitalis Blanka haule na Ofisa Tawala wa Wilaya ya Tarime, Bw. Egdi Mkwera ambaye alikuwa mtaalam wa mifugo


Aliyekuwa Mbunge wa Ludewa kwa tiketi ya CCM, Deogratias Filikunjombe, enzi za uhai wake.

Name:  f1.jpg
Views: 32143
Size:  54.0 KB
Helkopta (Chopa) iliyo anguka na kusababisha maafa hayo.

Historia fupi kuhusu Marehemu Deogratias Filikunjombe.
Deo Filikunjombe alimaliza shahada yake ya Mass Communication Makerere University Uganda
- Alikuwa Ripota wa Radio One na ITV kwa muda mrefu akitumia jina la " Deo Haule" akiripoti toka Kampala
- Alijiunga na Jeshi la Polisi na kufanya kazi kwa mwaka mmoja kisha akaacha kazi sababu alipangiwa kitengo cha Habari makao makuu ya Polisi na kufanya kazi chini ya Mohamed Mhina ambaye alikuwa chini yake kielimu.
- Alipotoka Polisi, alijiunga na World Vision kama Communication/ Information Officer na kufanya kazi kwa miaka kama minne hivi akiwa Makao makuu Arusha na baadae akahamishiwa tawi la dar es salaam
- Alipotoka World Vision akajiunga na MKURABITA ambapo alifanya kazi kwa muda usiozidi miaka miwili akaacha.
- Baada ya kuacha MKURABITA, akafungua duka lake la electronics lipo Benjamin Mkapa Tower, opposite na Posta Mpya ghorofa ya kwanza, akafungua vituo vyake vya kuuzia mafuta Ludewa na ndipo akaanza harakat.

chopa
Marehemu Deogratias Filikunjombe akiwaaga wananchi wake mapema alipoenda kufanya kampeni.

Uongozi wa blog ya kijana huru inatoa pole ya dhati kwa wafiwa wote na kwa chama cha mapinduzi, uongozi unatambua mchango mkubwa wa maendeleo uliokua unatolewa na  Mheshimiwa Filikunjombe na wote waliopata ajari, bwana ametoa naye ametwaa.

0 comments:

Post a Comment