18 Sept 2015

14-YEARS OLD BOY MISTAKENLY ARRESTED BY POLICE FOR HIS HOME MADE CLOCK (Kijana aliyekamatwa na polisi sababu ya kuhofiwa kutengeneza bomu)

Ni kijana anaye tambulika kwa jina la Ahmed Mohamed mwenye asili ya Sudan anayeishi Marekani,


Kijana huyo ambaye ni mwanafunzi wa masomo ya sayansi katika shule moja uko marekani hv majuzi alibuni saa kutoka kwenye vifaa baki vya ki electroniki ikiwa ni kazi ambayo mwalimu aliwapa wanafunzi kwenda kubuni kitu chochote cha kisayansi.
Baada ya kijana Ahmed kumaliza kazi yake ya kubuni saa hiyo, aliipeleka moja kwa moja shuleni kumuonesha mwalimu, ndipo kizaazaa kilipo ibuka baada ya mwalimu huyo kuhisi kifaa hicho ni bomu na ndipo kuwaita polisi ambao walimuweka rumande mpaka walipo fanya utafiti madhubuti na kugudua kua kifaa hicho si bomu bali ni saa iliyobuniwa na kijana huyo.


Baba wa mtoto huyo amesikitishwa na kitendo hicho na ata mtoto mwenyewe amepata hofu, lakini kwa mtazamo wa tofauti raisi Barack Obama amempongeza mtoto huyo na kumkaribisha ikulu na kusema Marekani imefika apo ilipo sababu ya vijana wabunifu na wanaojituma kama mtoto Ahmed nakuhaidi kukiendeleza kipaji hicho.
Kama vijana wakitanzania hasa tunaochukua masomoya sayansi tunatakiwa kujifunza kutoka kwa mtoto Ahmed ili kuendeleza  sayansi yetu na kuibua wataalamu wetu wenyewe ili kuendeleza nchi yetu.

0 comments:

Post a Comment