Mgodi wa wachimbaji wadogo wa nyangarata wilayani kahama, ulioporomoka.
Watu kumi
na moja wamenusurika kifo na wengine zaidi ya saba wanahofiwa
kufa baada
ya mgodi wa wachimbaji wadogo wa dhahabu wa Nyangarata wilayani Kahama
Shinyanga kuporomoka na kifusi kuwafukia huku wachimbaji waliobaki wakidai
kukosa msaada wa kuwaokoa wenzao walioko ardhini wakiomba msaada.
Wakizungumza
na waandishi wa habari, baadhi ya wachimbaji katika mgodi huo wameilalamikia
serikali kuwatelekeza bila msaada wowote huku wakidai kuwa hata uongozi wa
mgodi umeshindwa kuchukua hatua ili kuwaokoa wenzao waliofukiwa na kifusi.
Kwa
upande wake katibu mtendaji wa wachimbaji wadogo wilaya ya Kahama amekiri
kutokea kwa maporomoko hayo huku akidai kuwa tukio hilo limekua la kutatanisha
kwakuwa wakati linatokea watu walikuwa wakifanya kazi zao kama kawaida na
wanaohofiwa kufa kati yao wapo wataalamu wa uokoaji wanne wakiokuwa
wakijitahidi kuwaokoa wachimbaji hao.
Source: ITV
0 comments:
Post a Comment