8 Oct 2015

HARI YA UMEME TANZANIA YAZIDI KUA MBAYA, BWAWA LA MTERA LAFUNGWA RASIMI, SOMA HAPA KUJUA SABABU.

Ni dhahiri kua katika dunia ya sasa shughuli nyingi  za maendeleo zinategemea nishati umeme, na nishati hii inapokosekana basi maendeleo urudi nyuma kwa asilimia fulani, katika hali ya kusikitisha na kusononesha moja ya mabwawa tegemeo kwa uzalishaji wa umeme Tanzania linaloitwa Mtera lililoko kati ya mikoa ya Dodoma na Iringa lafungwa rasmi.

Bwawa la Mtera.

Bwawa hilo limefungwa baada ya shirika la umeme nchini, TANESCO kusimamisha uzalishaji wa umeme kwa kuzima mitambo iliyopo katika bwawa hilo kutokana na kupungua kwa kina cha maji katika bwawa hilo linalo zalisha megawati 80 ambacho ndicho kiwango cha juu kabisa kuzalishwa na bwawa moja hapa nchini.
Hayo yame thibitishwa na meneja wa TANESCO katika kituo hicho cha Mtera Mhandisi Abdallah Ikwasa baada ya kuzungumza na waandishi mbalimbali wa habari walio tembelea kituo hicho kujionea hali halisi, amesema hatua hiyo imechukuliwa kutokana na kupungua kwa maji kusiko kwa kawaida katika bwawa hilo ata kufikia hatua ya kuzalisha umeme chini ya mita za ujazo zinazo takiwa kitaalamu.

Baadhi ya wataalamu wakiangalia namna maji yalivyo pungua bwawa la Mtera.

Muhandisi huyo amesema kwa hali hiyo, tegemeo pekee la nishati ya umeme nchini ni mitambo ya uzalishaji umeme kwa kutumia gesi asilia ambayo shirika linaendelea kuimarisha vituo vya uzalishaji ili kuondoa hadha ya ukatikaji na mgao wa umeme unaoendelea kwa sasa kwa maeneo yaliyo unganishwa na gridi ya Taifa.

Source: ITV

0 comments:

Post a Comment