15 Sept 2015

GOLD EXTRACTION FROM FAECES( Uchimbaji wa Dhahabu kutoka kwenye Kinyesi)

Wahenga walisema, UKISITAHAJABU YA MUSA......,
Amini usiamini, wanasayansi nchini marekani wameanza mikakati ya kusafisha dhahabu kutoka kwenye kinyesi cha binadamu yaani MAVI.Wanasayansi hao wanadai kua madini hayo ya dhahabu na mengine mengi ya thamani na ambayo ni nadra kupatikana yameonekana kwa wingi katika vituo vya kusafishia vinyesi (mavi), na idadi ya madini hayo kupatikana kwa wingi ata zaidi ya kiasi kile wanachopata katika machimbo.

Kulingana na ripoti iliyo chapiswa katika kongamano la 249 la wakemia wa marekani (American Chemical Society,ACS) iliyo andikwa uko Denver Marekani, Ripoti hiyo inaeleza kua iwapo kutatambuliwa mbinu ya kusafisha kinyesi na kutenga dhahabu basi mbinu hiyo itasaidia sana mazingira, Daktari Kathleen alie saidia katika uandishi wa ripoti hiyo anadai kinyesi cha watu kina kiwango cha juu mno cha dhahabu, fedha, palladium na vanadium, madini hasa ya vanadium na shaba yanamanufaa makubwa sana katika utengenezaji wa bidhaa zinazotumika katika simu za mkononi na kompyuta mbali na bidhaa mbalimbali za kielektroniki.
Source:bbc swahili link>>http://www.bbc.com/swahili/habari/2015/03/150324_gold_feaces_usa

0 comments:

Post a Comment