9 Dec 2015

HUYU NDIE DR BEN CARSON, MTANZANIA ATAKAE GOMBEA URAISI MAREKANI MWAKA 2016 KUPITIA CHAMA CHA REPUBLICAN, MFAHAMU VIZURI HAPA.



Daktari Benjamin S. Carson

Yule daktari bingwa wa maswala ya Neurologia (nyurolojia) kwa watoto na pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Nyurolojia kwa watoto katika hospitali ya Johns Hopkins huko nchini Marekani Daktari Benjamin S. Carson ambaye ana asili ya kiafrika anayeishi Marekani amesema ana mpango wa kutembelea nchi ya Kenya kwa nia ya kutafuta asili yake, ambayo alisema amefatilia kwa ukaribu na kugundua kua asilia yake ya wazee wake yani wazazi wake wanatokea katika nchi mbili yani Kenya na Tanzania na wana asili ya kabila la wa Turkana ambao zaidi wanapatikana katika nchi ya Kenya na kiasi kidogo Tanzania.


Daktari Benjamin S. Carson ndie anaetegemewa kugombea kiti cha Uraisi katika nchi ya Marekani kupitia chama cha Republican hapo mwaka 2016.


Baadhi ya mambo makubwa ambayo Daktari Benjamin S. Carson alishawahi kutenda ambayo yalishangaza dunia ni pamoja na:
Mwezi wa tisa mwaka 1987, Carson alifanya upasuaji wa kutenganisha mapacha wenye umri wa miezi saba, waliokuwa wameungana katika sehemu ya kichwa. Carson alikuwa ndiye kiongozi wa upasuaji huo mgumu, Mwaka 1997, Carson pamoja na timu yake, walienda Afrika ya Kusini, kuwatenganisha Lukas na Joseph Banda kutoka Zambia. Watoto wote wawili waliweza kuishi baada ya upasuaji na hakuna hata mmoja wao aliyepata uharibifu wa ubongo. Watoto hao wa Banda walikuwa ni watoto wa kwanza walioungana kwa upande wa juu wa vichwa vyao kuweza kuishi baada ya upasuaji. Upasuaji huo ulifanyika kwa saa 28. Mwaka 2003, Carson alikuwa moja kati ya madaktari waliofanya upasuaji wa watu wazima waliokuwa wameungana katika sehemu ya vichwa, Ladan na Laleh Bijan. Lakini wote hawakuweza kuishi baada ya upasuaji. Alipoulizwa kwa nini alikubali kufanya upasuaji wa kubahatisha kiasi hicho alisema, ndugu hao walikwa wamekubali bora wafe kuliko kuendelea kuishi wakiwa wameungana.

 Bila kusahau Daktari Benjamin S. Carson ndie muandishi wa vitabu vya THINK BIG pamoja na GIFTED HANDS




0 comments:

Post a Comment