5 Dec 2015

HIZI NDIZO REKODI TANO ZA SOKA AMBAZO HAZIJAWAI KUVUNJWA KATIKA HISTORIA YA SOKA.

REKODI YA KWANZA
Idadi ya mashabiki wengi wa soka kuingia uwanjani:
 Hii ni rekodi iliwekwa katika mchezo wa fainali ya Kombe la Dunia mwaka 1950 katika mchezo kati ya Brazil dhidi ya Uruguay katika dimba la Maracanazo, mchezo ambao unatajwa kuingiza idadi rasmi ya watu 173,850 ila inatajwa kuwa idadi ilifikia hadi watu 210000 pamoja na wasio kuwa na tiketi.
World Cup Finals, 1950, Brazil, Rio De Janeiro, Aerial view of the gigantic Maracana Stadium still under construction for the 1950 World Cup finals  (Photo by Popperfoto/Getty Images)


REKODI YA PILI
Timu iliyowahi kufungwa magoli mengi zaidi: 
Rekodi hii iliwekwa mwaka October 31-2002 katika mchezo ngazi ya vilabu kati ya AS Adema dhidi ya SO l’Emyrne uliyochezwa Madagascar. Mchezo ulimalizika kwa AS Adema kuibuka na ushindi wa goli 149 – 0 magoli ambayo SO l’Emyrne walijifunga kwa makusudi baada ya mchezo uliyopita kutoridhishwa na maamuzi ya refa na kuwafanya wakose matumaini ya kutwaa ubingwa. Baada ya mechi kocha wa SO l’Emyrne alifungiwa miaka mitatu na wachezaji wanne walifungiwa hadi mwisho wa msimu.
149-0-1416147447R


REKODI YA TATU
Ali Daei, kutokea Iran amewahi kucheza katika vilabu vya Bayern na Hertha BSC na timu ya taifa ya Iran, anashika rekodi ya kufunga idadi kubwa ya magoli katika mechi za kimataifa, amecheza jumla ya mechi 149 akiwa na Iran na kufunga magoli 109 katika miaka 13 yake ya kucheza soka.
4-1416145061


REKODI YA NNE
Licha ya kuwa Pele ndio anatajwa kuwa mchezaji aliyecheza mechi nyingi 1375 kwa kila mechi, ila idadi ya mechi zake rasmi za mashindano zinatajwa kuwa 1115, golikipa Rogerio Ceni ndio mchezaji ambaye anatajwa kuwa amecheza mechi nyingi zaidi rasmi kuliko mchezaji yoyote, amecheza jumla ya mechi 1141. Ceni alikuwa akiichezea Sao Polo ya Brazil toka mwaka 1992. Rekodi ambayo inatajwa kaiweka akiwa na klabu moja na jumla ya mechi zake chache alizocheza timu ya taifa.
8-1416145035 (1)


REKODI YA TANO
Klabu ya Real Madrid ya Hispania ndio inatajwa kuwa na rekodi ya kuchukua Kombe la klabu Bingwa Ulaya mara tano mfululizo, imewahi kufanya hivyo mwaka 1955 na 1960. Licha ya kuwa Barcelona ya Guardiola na FC Bayern Munich ya Heynckes kutajwa kuwa bora haijawahi kutwaa taji hilo hata mara mbili mfululizo.
6-1416144968

Source: Millardayo.com

0 comments:

Post a Comment