14 Sept 2015

OVERVIEW ON NATIONAL ELECTION IN TANZANIA ( Mtazamo juu ya uchaguzi mkuu Tanzania)

Siku chache zimebaki kwa Tanzania kuingia katika uchaguzi mkuu ambao unausisha uchaguzi wa rais, wabunge na madiwani, kama mtanzania mwenye mapenzi mema na tanzania huu ni wakati sasa wa kutafakali rasimu za vyama mbalimbali ili mwisho wa siku kupata kujua kula yako itaelekea wapi.

Ni mambo mengi ambayo watanzania tunahitaji serikali ijayo ama viongozi wajao waweze kutenda ili kuleta mabadiliko chanya kwa nchi yetu hasa katika vipengele vya uchumi, afya, nishati na madini, kilimo na ufugaji. ajira, miundo mbinu, ujasiriamali pamoja na usimamizi na utendaji mathubuti ya mihimili mikuu mitatu ya nchi ambayo ni serikali, bunge na mahakama.

Hivyo basi kama kweli watanzania tunahitaji mabadiliko ya kweli ni wakati wetu sasa kusikiliza, kutathimini, kuchambua, kuamua na kuchagua viongozi sahii na si kuchagua kwa muonekano wa nje, kwa mgao wa pesa, viatu, kanga au tisheti bali kwa sera na utendaji.
Lakini tukumbuke mabadiliko na maendeleo ya nchi yeyote si tu huletwa na uongozi wa viongozi bora bali utendaji, bidii na kujituma kwa wananchi wa nchi hiyo, hivyo ni wajibu wetu hasa vijana kujiandaa kisaikolojia katika kujituma kwa kushirikiana na uongozi bora ili kuleta maendeleo tunayo yahitaji.
Nimalizie kwa kusema KAMA MTANZANIA USIHOJI NI NINI TANZANIA IMEFANYA KWAKO BALI JIULIZE NI KIPI UMEIFANYIA TANZANIA YAKO, nawatakia uchambuzi mzuri wa rasimu za vyama na pia tusiache kujitokeza kwa wingi katika kupiga kura tarehe 25 mwezi wa 10 mwaka 2015, kumbuka kiongozi unayemtaka ataletwa na kura yako mwenyewe.






0 comments:

Post a Comment