20 Sept 2015

ALL YOU ARE SUPPOSED TO KNOW ABOUT U.T.I DISEASE ESPECIALLY TO CHILDREN AND YOUTH ( Ujue vizuri ugonjwa wa U.T.I hasa kwa watoto na vijana wa lika na jinsia zote)

MAANA YA U.T.I
U.T.I kirefu chake ni URINARY TRACK INFECTION au kwa lugha nyepesi tunaweza kusema ni maambukizi kwa njia ya mkojo.
 Ugonjwa huu husababishwa na bakteria anayeitwa Escherichia coli (E. coli) ambao makazi yao ya kawaida ni kwenye utumbo mpana, hivyo huwa wanapatikana pia kwenye haja kubwa. Lakini baadhi ya watu wanaweza kupata tatizo hili kutokana na kuingiwa na fangasi ingawa pia zipo sababu nyingine chache. 
Bakteria wa Escherichia coli hawasababishi peke U.T.I bali huambatana na wengine waitwao staphylococcus, saprophyti cus, pseudom onas, enterobacter na kadhalika na maambukizi katika njia ya mkojo mara zote yanatokea kwenye njia ya mkojo na si pengine popote.





VYANZO VYA U.T.I
1.Maji machafu,matumizi ya maji machafu wakati wa kujisafisha huweza kuweka bacteria kwa urahisi na kusababisha U.T.I

2.Vyoo kuwa vichafu,pia matumizi ya vyoo ambavyo ni vichafu huweza kusababisha kupata U.T.I kwa sababu ndani ya choo kuna bakteria wengi amabao sababisha U.T.I.

3.Ngono,kufanya ngono mara kwa mara ni tatizo kubwa ambalo huweza kusababisha U.T.I sababu wakati wa ngono msuguano hua mkubwa ambao hufanya bacteria kutoka kupitia maji maji ya ukeni na kuingia katika njia ya mkojo,mtu ambae anafanya ngono mara kwa mara yuko kwenye hatari ya kupata U.T.I kuliko yule ambae hafanyi ngono mara kwa mara.

4.Kuvaa nguo za mitumba bila kufua, matumizi ya nguo za mtumba bila kufua husababisha kwa urahisi kupata U.T.I sababu ya bakteria waliomo kwenye nguo hizo.

6.Kemikali, hili ndo tatizo kubwa hasa kwa wanawake wengi ambao siku hizi utumia saana kemikali hasa kwenye vipodozi ambapo kemikali hizi kwa kuwa ni sumu huenda hadi kwenye kibofu na kuchubua kibofu na kua chanzo cha U.T.I

7.Kubana mkojo kwa muda mrefu,pia kubana mkojo kwa muda mrefu kunaweza sababisha U.T.I.

KINGA ZIDI YA U.T.I
Kwa Wanawake,  wanashauriwa kuepuka kujisafisha sehemu za siri na maji machafu na yasiyo salama, pia kuepeuka kupaka marashi sehemu hizo, ama kutumia pamba zenye kemikali ya kukata harufu kwani hizo huua bakteria wa asili wa ukeni hali ambayo hukaribisha bakteria wa maradhi kuzaliana kwa wingi. Pia wanashauriwa wanapojisafisha baada ya kujisaidia kuanzia mbele kwenda nyuma, ili kuepusha kuhamisha bakteria walio eneo la haja kubwa na kuingia njia ya mkojo.
Kwa ujumla, unaweza kuudhibiti au kuponya ugonjwa huu kwa kunywa maji mengi pamoja na juisi itokanayo na matunda halisi, iwapo tutawahi kabla tatizo halijawa sugu. Kwa maana nyingine, unaweza kujikinga na ugonjwa huu kwa kuwa na mazoea ya kunywa maji ya kutosha kila siku. Ukinywa maji ya kutosha yatakufanya uende haja ndogo kila mara na kwa njia hiyo wale bakteria watakuwa wakitoka na hatimaye kuisha kabisa. 

DALILI ZA U.T.I
1.Mwili kuchoka mara kwa mara
2.Homa ya mara kwa mara
3.Kichwa kuuma mara kwa mara
4.Kubanwa na mkojo halafu ukienda kukojoa unakuta mkojo kidogo
5.Maumivu wakati wa kukojoa hasa kipindi cha kumalizia mkojo
6.Kiuno kuuma.

MATIBABU YA U.T.I
Matibabu ufanyika mara baada ya kufanyiwa vipimo na kuthibitika kuwa mgonjwa ana maambukizi  ya U.T.I. Dawa ambazo anaweza kupewa ni kama vile Ciprofloxacin, Monurol, Furadantin, Sulfam ethoxazole, co-trimax, ampicillin, gentamicin na kadhalika. Mgonjwa anayesumbuliwa na U.T.I hapaswi kutumia dawa yoyote bila kwanza kupata ushauri wa daktari.
MADHARA YA U.T.I
Kwa wanaume, maambukizi haya huathiri nguvu za kiume maana bakteria  hujipenyeza hadi katika korodani na huathiri uzalishaji wa mbegu za kiume na kunaweza hata kusababisha ugumba. Hivyo unashauriwa kuhakikisha unatibu bila kuchelewa ugonjwa huu. 
Pia maambukizi ya njia ya mkojo huweza kusababisha matatizo ya tezi ya kiume (prostate) kwani husababisha mrija wa mkojo kuziba, kutopitisha mkojo vizuri na kuruhusu bakteria kujenga makazi. Hali hiyo ikitokea mgonjwa lazima akamuone daktari ili awekewe mrija wa kutolea mkojo.

MWISHO
Afya ya mwili ni kitu cha muhimu sana maana kinachangia katika ufanisi wa uzalishaji mali na maendeleo katika jamii, hivyo sote tunatakiwa kujali afya zetu kwa kufanya mazoezi, kula vizuri na kunywa maji ya kutosha, kupata muda mzuri wa kupumzika na ata wakati wa kulala pia kufanya shuguli zetu za maendeleo katika sehemu salama.




0 comments:

Post a Comment