20 Sept 2015

KENYAN GOVERNMENT FAIL TO PAY THEIR TEACHERS (Serikali ya Kenya imekataa kulipa madai ya Walimu nchini humo)

Ikiwa ina fahamika kua walimu ni watu wa muhimu sana katika jamii yeyote ile kutokana na kazi yao ya kusambaza taaluma katika jamii, na kuweza kuzalisha wataalamu ambao ni chachu ya maendeleo.
Uko kenya, baada ya muda mrefu wa malumbano na migomo  ya walimu wakidai malipo yao na kupelekea shula zote za umma na binafsi kufungwa, Raisi wa nchi hiyo Mh, Uhuru Kenyatta katika hotuba yake kwa njia ya televisheni amesema na kusisitiza kua serikali ya nchi hiyo haina uwezo wakulipa madai ya nyiongeza ya mishahara walio kuwa wanadai walimu wanao endelea na migomo.

Baadhi ya walimu katika mgomo.

Raisi huyo ametoa wito kwa mgogoro huo kutatuliwa kwa amani, na serikali ya nchi hiyo kuagiza shule zote nchini humo kufungwa na wanafunzi kurudi nyumbani, ambapo watakao bakia pekee ni wale wanaojiandaa na kufanya mtihani wa taifa wa darasa la nane na kidato cha nne mwaka huu.
Mahakama nchini humo inatarajia kuamua ivi karibuni iwapo mgomo huo wa walimu ni halali au si halali.

Raisi wa Kenya Mh,Uhuru Kenyatta

Source:bbc swahili

0 comments:

Post a Comment