Kamati ya kutafuta ukweli ya Umoja wa
Mataifa kuhusu Syria imetangaza katika ripoti yake iliyotolewa Alkhamisi tarehe
3 Septemba kwamba Syria inasumbuliwa na mgogoro unaotokana na maslahi ya
kijiografia ya madola ya kigeni. Ripoti hiyo imesema kuwa: Vita vya Syria
vilianzishwa kwa ajili ya kudhamini maslahi ya baadhi ya nchi za kanda hiyo na
za kimataifa.
Hapana shaka kuwa,
kifungu hiki cha ripoti ya kamati ya kutafuta ukweli ya Umoja wa Mataifa kuhusu
vita vya ndani nchini Syria kinaashiria Marekani, nchi za Ulaya na washirika
wao wa Mashariki ya Kati kama Saudi Arabia, Qatar, Uturuki na utawala haramu wa
Israel. Ripoti hiyo ya kamati ya Umoja wa Mataifa ambayo imetayarishwa kwa
kutegemea mahojiano 355, nyaraka za kitiba, picha za satalaiti na jinai kubwa
kama za mauaji, ubakaji, kutekwa nyara watu na uharibifu mkubwa uliofanyika
nchini Syria katika kipindi cha miezi sita ya kuanzia Januari mwaka huu,
imeitaka jamii ya kimataifa kuwapokea wakimbizi wa Syria na kuzuia maafa
makubwa zaidi ya kibinadamu katika nchi hiyo.
Tangu mwaka 2011
Syria ilitumbukizwa katika vita vinavyoendeshwa na nchi za Magharibi zikiongozwa
na Marekani. Wasyria ambao wanataabika kutokana na vita hivyo wanalazimika kuwa
wakimbizi nchini mwao au kukimbilia katika nchi jirani na barani Ulaya.
Inaripotiwa kuwa katika mwaka huu wa 2015 pekee zaidi ya Wasyria 2500
wamefariki dunia katika maji ya Bahari ya Mediterania wakikimbia ukatili wa
makundi ya kigaidi kama Daesh. Maiti za wakimbizi hao zinazoopolewa baharini au
kuokotwa katika pwani ya nchi kama Uturuki zimewatia simanzi na huzuni watu
wengi duniani. Kamisheni Kuu ya Wakimbizi ya Umoja wa Mataifa inakadiria kuwa
Wasyria zaidi ya milioni nne wamekimbia nchi yao na imetahadharisha kuhusu
maafa makubwa yanayotokea nchini humo.
Hapana shaka kuwa,
mgogoro wa Syria ndio mbaya zaidi wa kibinadamu katika karne hii ya 21 na kwa
mujibu wa Kamisheni Kuu ya Wakimbizi ya Umoja wa Mataifa, dunia haijawahi
kukumbana na mgogoro mkubwa na mbaya kama huu katika kipindi cha miaka 25
iliyopita. Ripoti zinasema kuwa, nusu ya wakazi wote wa Syria wamepoteza makazi
yao katika kipindi cha miaka 4 iliyopita na wengi miongoni mwao wamelazimika
kuishi ukimbizini.
Zaidi ni kwamba
vita hivyo vilivyopangwa na nchi za Magharibi vimezaa matunda mabaya zaidi na
wanaharamu makatili kama makundi ya kigaidi ya Daesh na Jabhatu Nusra, mauaji
ya kizazi na kuharibiwa turathi za Syria zenye umri wa maelfu ya miaka.
Utumiaji wa silaha
zilizopigwa marufuku unaoshuhudiwa Syria kama gesi ya haradali na mabomu ya
kemikali umesababisha maafa makubwa sana ambayo yatakuwa na taathira mbaya kwa
Syria na kanda nzima ya Mashariki ya Kati kwa miaka mingi hata baada ya nchi
hiyo kurejea katika hali yake ya kawaida.
Wakati huo huo
kimya cha jamii ya kimataifa na kutowajibika Umoja wa Mataifa kumezidisha
mgogoro wa Syria na ripoti ya kamati ya kutafuta ukweli iliyoundwa kufuatilia
suala hilo imethibitisha uhakika huo.
Baadhi ya wakimbizi kutoka syria wakiwa na mizigo yao
Namna uaribifu unavyo tokea uko syria.
source; iranSwhiliRadio (IRIB World Services)
0 comments:
Post a Comment