• HIZI NDIZO SABABU ZINAZOPELEKEA WAPENZI WENGI KUTOKUA WAAMINIFU

  • HII NDIO TARIFA WALIOTOA WATALAMU WA JIOLOJIA (GST) JUU YA TETEMEKO LA ARDHI MKOANI KAGERA

  • TOKA TCU, CHEKI HAPA KAMA UMECHAGULIWA KUJIUNGA NA CHUO KWA MWAKA WA MASOMO 2016/2017

  • HIZI NDIZO MBINU 6 KUBWA ZITAKAZO KUSAIDIA KUPATA AJIRA MAPEMA NA KWA URAHISI

  • MAMBO 7 YA KUFANYA UNAPOKUWA KATIKA NYAKATI NGUMU ZA KIMAISHA

6 Jan 2017

HII NDO LIST YA WASHINDI WA TUZO ZA CAF KWA MWAKA 2016, CHEKI HAPA

Image result for Caf AWARD
January 5 2017 Abuja Nigeria ndio ilifanyika hafla ya utolewaji wa tuzo za soka za mwaka 2016 na shirikisho la soka barani Afrika Caf, tuzo hizo ambazo utolewa kwa wachezaji waliyofanya vizuri kwa mwaka husika kwa kupigiwa kura


  • Riyad Mahrez wa Algeria na Leicester City ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa Afrika 2016 amewashinda Mane na Aubameyang

Image result for riyad mahrez 2015

  • Golikipa wa Uganda na Club ya Mamelodi Sundowns Denis Onyango ameshinda tuzo ya mchezaji bora Afrika kwa Ligi za ndani

Image result for Denis Onyango
Denis Onyango

  • Bakary Papa Gassama wa Gambia ameshinda tuzo ya refa bora wa mwaka 2016

Image result for Bakary Papa Gassama
Bakary Papa Gassama

  • Mchezaji wa Nigeria Asisat Oshoala ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa kike kwa mwaka 2016 

Image result for Asisat Oshoala
Asisat Oshoala

  • Uganda The Cranes imeshinda tuzo ya timu bora ya taifa ya wanaume kwa mwaka 2016

Image result for Uganda The Cranes
Uganda The Cranes 

  • Kocha wa Mamelodi Sundowns Pitso Mosimane ameshinda tuzo ya kocha bora wa mwaka 2016

Image result for Pitso Mosimane
Pitso Mosimane

  • Staa wa Arsenal na Nigeria Alex Iwobi ameshinda tuzo ya mchezaji bora kijana kwa mwaka 2016

Image result for Alex Iwobi
Alex Iwobi

  • Staa wa ManCity na timu ya taifa ya Nigeria Kelechi Iheanacho ameshinda tuzo ya Most Promising talent 2016

Image result for Kelechi Iheanacho
 Kelechi Iheanacho

  • Mabingwa wa Club Bingwa Afrika Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini wameshinda tuzo ya Club bora ya mwaka 2016

Image result for Mamelodi Sundowns
Mamelodi Sundowns

  • Timu ya taifa ya wanawake ya Nigeria imeshinda tuzo ya timu bora ya mwaka 2016 ya wanawakeImage result for Nigeria WOMEN TEAMTimu ya taifa ya wanawake ya Nigeria

5 Jan 2017

PENZI LA HARMONIZE NA WOLPER KUSHINEI, CHEKI HAPA

hamon-na-wolper
NGULI wa sanaa ya maigizo wa Bongo ajulikanaye kama Jeniffer Lopez wa Bongo,  mrembo Jacqueline Wolper ‘Gambe’ na msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka lebo kubwa ya muziki Bongo, Harmonize, penzi lao lineaendelea kudhihirika wazi kuwa ni penzi la maigizo.


wolper-1
Wawili hao licha ya kuwa penzi lao lilikosa kuaminiwa na wengi tokea awali, waliendelea kuonyesha wazi kuwa wameshibana na wameamua kuwa pamoja. Mwaka jana katika mitandao ya kijamii ziliwekwa picha na wawili hao wakiwa sehemu mbalimbali kama vile katika shoo kadhaa huko Mtwara, mbuga za wanyama na sehemu zenye kulipa uhai pendo.

wolper-2
Januari 5 mwaka huu wawili hao wameianza siku katika hali ya utata ikiwemo kufuta picha za pamoja katika mitandao ya kijamii na Wolper kuandika maneno haya instagram:

“Nina akili timamu me syo mtoto endelea na maisha yako It is over sasa waambie rasmi usifiche tena @harmonise_tz I hate love”.

Source:Global publishers/Salum Milongo

16 Sept 2016

HIZI NDIZO SABABU ZINAZOPELEKEA WAPENZI WENGI KUTOKUA WAAMINIFU.

Image result for black people cheating in relationship

Huwa inatokea ambapo wanaume na wanawake hutembea na watu zaidi ya mmoja na ni kitu ambacho sote tunafahamu na tumeona na kama haujaona basi utakua umesikia tetesi.

Wanawake kutembea na wanaume wengi ni aibu na pengine inaweza kupelekea jamii kukunyanyapaa tofauti kwa wanaume na hofu hii huchangia kwa wanawake kua waaminifu na kutulia na wapenzi wao.

Linapokuja suala la biolojia ya uzazi, Wanaume wanaweza kuzalisha mamilioni ya mbegu kwa siku, tofauti na wanawake ambao takribani yai moja urutubishwa kila baada ya siku 28.

Kutokana na sababu za kibiolojia , wanaume wanaweza kurudia kushiriki katika uzazi mara nyingi zaidi kuliko wanawake hivyo hii huleta uraisi kwa wanaume kuweza kua na wanawake wengi zaidi.

Mara nyingi watu huwa na ugumu wa kuelewa dhana ya upendo na tamaa. Kama upo na mtu kwa kumtamani tu mara nyingi unapopata nafasi ya kulala nae na kupata kumjua zaidi  humkinai ndipo inapotokea mtu kutafuta uhusiano mwingine na kusababisha udanganyifu na kutembea na wanawake au wanaume wengi (kua kicheche).

Uwezekano wa kufikiria kuachana na mwenzi wako baada ya kutembea nae ni ndogo kwa wanawake tofauti na wanauume ambapo mwanawake akitembea na mwanaume hushirikisha zaidi hisia na moyo nakusababisha kujikuta kupenda kwakupitiliza.

Hivi ni baadhi ya vitu ambavyo mwanamke au mwanaume unatakiwa kumchunguza mwenza wako kwasababu akiwa navyo husababisha kutokua muaminifu (kicheche).

  • Kama hajiamini
  • Ana akili za kitoto
  • Ameathirika na mapenzi kabla(kuumizwa)
  • Hajui kuhusu mapenzi
  • Anaugonjwa wa ngono
  • Mtumiaji wa madawa ya kulevya n.k

15 Sept 2016

TOKA TCU, CHEKI HAPA KAMA UMECHAGULIWA KUJIUNGA NA CHUO KWA MWAKA WA MASOMO 2016/2017

Image result for tcu tanzania

Sasa unaweza kuhakikisha (confirm) kama ni mmoja kati ya waliochaguliwa kujiunga na masomo ya chuo kwa mwaka wa masomo 2016/2017 kwakubonyeza link hii>>http://cas.tcu.go.tz/users/login

HILI NDILO TAMKO LA SERIKALI YA TANZANIA KUHUSU MADEREVA KUTEKWA HUKO CONGO, CHEKI HAPA.


1
2
Cheki video hapa chini....


Chanzo: Globalpublishers.com

MADEREVA KUTOKA TANZANIA WATEKWA NA WAASI HUKO CONGO, CHEKI HABARI NZIMA HAPA.

whatsapp-image-2016-09-15-at-8-34-33-am-750x375
Baadhi ya magari yanayodaiwa kuchomwa moto.

Chama cha Wamiliki wa Magari ya Mizigo nchini Tanzania (TATOA) kinaripoti kwamba, waasi wa Mai Mai nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), wamewateka nyara madereva wa Tanzania na kuchoma baadhi ya magari ya mizigo. Waasi hao wanadai dola za Kimarekani elfu nne (karibu shilingi za Kitanzania milioni tisa) kwa kila dereva ama sivyo watawapiga risasi madereva wote. Pia waasi hao wametoa siku ya mwisho (deadline) ya majeshi yanayolinda amani nchini humo kuondoka.

TATOA inasema imezungumza na mmiliki wa kampuni ya Simba Logistics,  Azim Dewji,  ambaye amethibitisha taarifa hizi na pia balozi wa Tanzania DRC  na Wizara ya Mambo ya Nje.  Serikali inashughulikia suala hili. Jumla ya magari yaliyotekwa ni 12 kati ya hayo magari 8 ni ya Tanzania na 4 ya Kenya. Magari 4 ya Tanzania yamechomwa moto na madereva wote walichukuliwa na waasi lakini bahati nzuri madereva wawili wa Tanzania walifanikiwa kuwatoroka. Tukio hilo limetokea sehemu inayoitwa Kasebebena na Matete, wastani wa kilomita 30 kutoka mji wa Namoya.

TATOA inawashauri wanachama waliopakia mzigo kuelekea huko kuwasiliana na madereva wao ili wasitishe safari, kusubiri taarifa ya hali ya usalama kutolewa.

Mai Mai Kata ni kundi la waasi nchini DRC ambalo linadai kupigania uhuru wa jimbo la Katanga, na linaongozwa na Gédéon Kyungu Mutanga, ambaye aliunda kundi hilo mara tu alipotoroka kutoka gerezani mwaka 2011.

Chanzo: Globalpublishers.com

13 Sept 2016

HARAMBE KUCHANGIA WAATHIRIKA KAGERA, WANANCHI WAONESHA MOYO WAKUJITOLEA, CHEKI HAPA.

Waziri mkuu mheshimiwa Kassim Majaliwa ameongoza harambe maalum iliyofanyika jijini Dar es Saalm ikiwakutanisha mabalozi mbalimbali wanaowakilisha nchi zao hapa nchini, umoja wa wafanyabiashara na mtu mmoja mmoja aliyeguswa na tukio la tetemeko la ardhi mkoani Kagera lililopelekea maafa makubwa yakiwamo mauaji na uharibifu wa miundombinu.
waziri-mkuu-kassim-majaliwa-2
Waziri mkuu Mh. Kassim Majaliwa akiongoza Harambe Kuchangia Waathirika Kagera
Kwenye harambe hiyo iliyoudhuriwa pia na waziri wa viwanda na biashara mheshimiwa Charles Mwijage jumla ya pesa zilizochangwa ni shilingi za kitanzania 1,396,000,000/=.

Pesa hizo taslimu na ahadi zilizotolewa na wageni mbalimbali waalikwa. Ambapo zimetolewa katika mafungu yafuatayo milioni 700, milioni 600, Euro 10,000 na Dola 10,000 na kufanya jumla yake kuwa 1,396,000,000/= kwa pesa za Tanzania.

Pia wafanyabiashara wakubwa wa makampuni matatu tofauti wameungana na kuahidi kukamilisha ukarabati wa shule za sekondari za Ihungo na Nyakato ndani ya siku thelathini kuanzia leo, makampuni hayo ni Oil Com, GPP na Moyo Group.

Baadhi ya wafanyabiashara waliochangia michango yao ni pamoja na Regnald Mengi (Milioni 110), umoja wa wauza mafuta ya rejereja (Milioni 250), Kiwanda cha sukari  Kagera (Milioni 100), IPTL (Milioni 100), China (Milioni 100) Dewji Foundation (Milioni 100), Mambo ya Nje (Milioni 10), Azania (Milioni 20).

Jumla ya fedha na ahadi zilizotolewa kuwasaidia waathirika tetemeko la ardhi ni takribani Sh1.4 bilioni pamoja na vifaa vya ujenzi.

Chanzo: Globalpublishers.com