Huwa inatokea ambapo wanaume na wanawake hutembea na watu zaidi ya mmoja na ni kitu ambacho sote tunafahamu na tumeona na kama haujaona basi utakua umesikia tetesi.
Wanawake kutembea na wanaume wengi ni aibu na pengine inaweza kupelekea jamii kukunyanyapaa tofauti kwa wanaume na hofu hii huchangia kwa wanawake kua waaminifu na kutulia na wapenzi wao.
Linapokuja suala la biolojia ya uzazi, Wanaume wanaweza kuzalisha mamilioni ya mbegu kwa siku, tofauti na wanawake ambao takribani yai moja urutubishwa kila baada ya siku 28.
Kutokana na sababu za kibiolojia , wanaume wanaweza kurudia kushiriki katika uzazi mara nyingi zaidi kuliko wanawake hivyo hii huleta uraisi kwa wanaume kuweza kua na wanawake wengi zaidi.
Mara nyingi watu huwa na ugumu wa kuelewa dhana ya upendo na tamaa. Kama upo na mtu kwa kumtamani tu mara nyingi unapopata nafasi ya kulala nae na kupata kumjua zaidi humkinai ndipo inapotokea mtu kutafuta uhusiano mwingine na kusababisha udanganyifu na kutembea na wanawake au wanaume wengi (kua kicheche).
Uwezekano wa kufikiria kuachana na mwenzi wako baada ya kutembea nae ni ndogo kwa wanawake tofauti na wanauume ambapo mwanawake akitembea na mwanaume hushirikisha zaidi hisia na moyo nakusababisha kujikuta kupenda kwakupitiliza.
Hivi ni baadhi ya vitu ambavyo mwanamke au mwanaume unatakiwa kumchunguza mwenza wako kwasababu akiwa navyo husababisha kutokua muaminifu (kicheche).
- Kama hajiamini
- Ana akili za kitoto
- Ameathirika na mapenzi kabla(kuumizwa)
- Hajui kuhusu mapenzi
- Anaugonjwa wa ngono
- Mtumiaji wa madawa ya kulevya n.k
0 comments:
Post a Comment