22 Aug 2016

HII NDO TAARIFA YA POLISI DAR KWA WANAO JIUSISHA NA 'UKUTA'

Kamanda wa Polisi kanda maalum ya Dar es salaam Simon Sirro

Licha ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kutangaza kufanya maandamano ya nchi nzima Septembe 1 2016, Jeshi la Polisi kanda maalum Dar es salaam limemkamata mtu mmoja anayejulikana kwa jina la Yoram Mbyellah kwa kupatikana na kuuza sare aina ya fulana zenye maneno yanayodaiwa kuwa ni yakichochezi zikiwa na alama ya CHADEMA huku nyingine zikiwa na maneno ‘UKUTA’

Kamanda wa Polisi kanda maalum ya Dar es salaam Simon Sirro amesema…"August 20 2016 Jeshi la Polisi lilipata taarifa toka kwa raia wema kuwa maeneo ya Kinondoni kuna duka linauza flana zenye maneno ya uchochezi yaliyoandikwa ‘’TUJIPANGE TUKATAE UDIKITETA UCHWARA’’ , ‘UKUTA’ "
"Aidha Polisi baada ya kupata taarifa hizo walifika eneo la tukio na kumkamata mtuhumiwa aitwaye YORAM SETHY MBYELLAH miaka 42, mfanyabiashara na mkazi wa Mburahati akiwa anauza fulana hizo dukani kwake" –Kamanda Sirro
"Ili tuishi kwa amani ni lazima tutii sheria na kama hutaki kutii sheria tutashughulika naye, Kama kuna mtu anataka kuvunja amani katika mkoa wetu ajue kabisa hatoweza na niseme tu kwamba kama wanataka kujenga ukuta wajenge ukuta mwingine maana huu umeshadondoka" –Kamanda Sirro
"Na wapo watu wanasema kwanini tunafanya mazoezi, nikwamba Jeshi la Polisi ni kawaida kufanya hivyo na muhimu watu wajue hiyo September 1 hakutakuwa na maandamano ya aina yoyote kwahiyo watu wasiwe na hofu bali wachape kazi" –Kamanda Sirro

Chanzo: millardayo.com

0 comments:

Post a Comment