22 Aug 2016

KWA SAMATTA HUYU WAZUNGU LAZIMA WASIMAME, CHEKI ALIYO FANYA.

Mbwana Samatta
Baada ya mtanzania Mbwana Samatta kuingoza timu yake ya KRC Genk kucheza mchezo wa kwanza wa round ya mwisho wa kuwania kufuzu hatu ya Makundi ya UEFA Europa League dhidi ya Lokomotiva ya Croatia na mchezo kumalizika kwa sare ya goli 2-2.  

August 21 2016 alishuka dimbani    kucheza mchezo wao wa nne wa Ligi Kuu Ubelgiji dhidi ya Lokeren katika uwanja wa Diknam unaotumiwa na Lokeren kama uwanja wa nyumbani, Samatta amefanikiwa kuiongoza Genk kuibuka na ushindi  wa goli 3-0 huku akifanikiwa kufunga magoli mawili dakika ya 34 na 38 kabla ya mjamaica Leon Bailey kufunga goli la mwisho dakika ya 48, Genk sasa inakuwa inafikisha jumla ya point 7 na kuwa nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi kuu Ubelgiji.

Mbwana Samatta
Kwa mchezo huo, Mbwana Samatta atakua kafikisha jumla ya magoli manne katika michezo yao minne ya Ligi Kuu waliyocheza msimu huu nakuongoza kwa kua mchezaji mwenye magoli mengi zaidi, angalia orodha ya top scorers katka ligi hiyo, hapa chini..

0 comments:

Post a Comment