Hassan Kessy
Beki wa pembeni wa Timu ya Yanga, Hassan Kessy amewaomba radhi wanachama na mashabiki wa timu hiyo baada ya kukosa penati katika mchezo wa kuwania ngao ya jamii iliyo chezwa kati yao na timu ya Azam.Kessy alisema kitendo cha kukosa penati kilimuumiza na mbaya zaidi ni pale alipo shuudia timu yake ikipoteza ubingwa huo waliokua wakiushikilia, aliongeza kusema anaomba mashabiki wamsamehe na wawasamehe timu nzima kwakua wanafahamu wameumia kwa matokeo hayo kwakua walikua na nafasi ya kushinda ila hawakua na bahati.
Hassan Kessy akifanya yake
Ikumbukwe mechi hiyo ilichezwa jumatano ya tarh 17/8/2016 ambapo Yanga na Azam walitoka suluhu ya mabao 2-2 iliyo wapeleka kwenye penati ambapo Azam iliifunga Yanga kwa mabao 4 kwa 1 bao lililofungwa na kipa wa Yanga aitwae Dida.
Timu ya Azam ikishangilia kwa furaha baada ya kuibuka mabingwa
0 comments:
Post a Comment