4 Feb 2016

HUU NDIO UKWELI KUHUSU MWANADADA, MWANAFUNZI MTANZANIA ALIE ZALILISHWA KWA KUVULIWA NGUO HUKO INDIA.

Kundi la watu lilimshambulia na kumvua nguo mwanafunzi wa kike mwenye umri wa miaka 21 baada ya mwanafunzi mmoja kutoka Sudan kumgonga na kusababisha kifo cha wanamke mmoja, siku ya Jumapili.
Mwanafunzi huyo wa kike pamoja na marafiki zake watatu wote kutoka Tanzania walikuwa wakipita tu katika eneo la tukio hilo, waliposhambuliwa na kuzalilishwa.

Picha kutoka maktaba.

SERIKALI YATOA TAMKO
Serikali imesema kuwa inaendelea kufuatilia ili kuchukua hatia zaidi juu ya matukio yalitokea nchini India katika chuo cha Acharya Bangalore, ikiwemo la mwanafunzi wa Kike kudhalilishwa kwa kuvuliwa nguo.
Akitoa tamko la Serikali leo Bunge Mjini Dodoma, Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Agustino Maige amesema tayari serikali imeshapeleka dokezi la kidiplomasia kwa serikali ya india ili kuonyesha kukasirishwa na kitendo hicho.
Balozi Maige ameongeza kuwa tayari wameitaka serikali ya India kuchukua hatua za kipolisi kufanya uchunguzi juu ya tukio hilo ikiwa ni pamoja na kupeleka ulinzi wa kutosha katika maeneo wanaoishi wanafunzi hususani wa kitanzania.
Mahiga
Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Agustino Mahiga.

WAHUSIKA WAKAMATWA
Wakati huo huo Wanaume wanne wanao tuhumiwa kuhusika katika kumshambulia na kumvua nguo mwanafunzi wa kike kutoka Tanzania wamekamatwa, shirika la habari la AP limeripoti.
Waziri wa mashauri ya kigeni wa India Sushma Swaraj, aliandika kwenye Twitter kwamba amesikitishwa sana na “kisa hicho cha aibu” kilichotokea Jumapili eneo la Bangalore.

1 comments: