28 Jan 2016

WATANZANIA WAHUZUNIKA BAADA YA SERIKALI KUTOA KAULI YA TBC KUTOONESHA TENA BUNGE LIVE, MKASA MZIMA HAPA.


Askari wakituliza ghasia ndani ya bunge

Vurugu kubwa zimetokea ndani ya ukumbi wa bunge na kusababisha kundi la polisi wa kutuliza ghasia kuingia ndani ya ukumbi huo na kuwatoa wabunge wa upinzani ambao walikuwa wanapinga kauli iliyotolewa na waziri wa habari, utamaduni, wasanii na michezo ya kutaka vikao vya bunge kufanyika bila ya kurushwa moja kwa moja na luninga ya shirika la utangazaji nchini (TBC).

Mvutano huo ulianza mapema asubuhi baada ya waziri mwenye dhamana husika kuwasilisha kauli yake bungeni kuhusu matangazo hayo hatua ambayo iliharibu hali ya hewa na kusababisha kikao kuahirishwa ili kutoa mwanya wa kamati ya uongozi kukaa na kufanya maamuzi.

Waziri wa habari, utamaduni, wasanii na michezo Mh Nape Nnauye.

Hata hivyo bunge hilo lilirudi kwenye kikao chake cha jioni ambapo hali ilizidi kuwa mbaya baada ya mwenyekiti Chenge kutangaza kuwa kamati ya uongozi ya bunge imesema ratiba ya kikao cha bunge iendele kama kawaida na ndipo hali ikanza hivi.

Tafurani hiyo ikadumu kwa muda mrefu na ndipo polisi wakaingia  ndani kwa lengo la kuwatoa nje wabunge.

Kama vile haitoshi hata waandishi wa habari nao walitolewa nje na mkuu wa kitengo cha habari elimu na mawasiliano kwa umma Bw Owen Mwandumbya hatu ambayo ili walazimu wanahabari kushindwa kutekeleza majukumu yao.

Awali kabla ya vurugu hizo baadhi ya wabunge wamepokea kwa mitizamo tofauti kauli ya serikali.

Badhi ya wabunge ambao ni wana taaluma ya habari wamesema kitendo cha kuzuia kutangaza bunge ni hatua ya mwanzo ya kuua uhuru wa habari nchini na hivyo serikali inabidi kujitazama upya.

0 comments:

Post a Comment