28 Jan 2016

KIVUKO CHA MV KILOMBERO CHAZAMA, IDADI YA WATU ISIYO FAHAMIKA WAHOFIWA KUFA MAJI, HABARI KAMILI HAPA.


Kivuko cha Mv Kilombero

Idadi ya watu isiyo fahamika mara moja wanahofiwa kufa maji yakiwemo magari matatu kudumbukia baada ya kivuko cha MV 2 Kilombero kuzama katikati ya mto Kilombero kufuatia upepo mkali ulioambatana na mvua kubwa kunyesha majira ya saa moja na nusu hadi saa tatu usiku.

chombo cha habari kimefika katika tukio hilo na kukuta umati wawatu huku jitihada za kufanya uokozi zikiendelea ambapo kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wamesema mvua kubwa iliyonyesha ikiambatana na upepo mkali uliosababisha kupasuka kwa injini moja ya kivuko na kusababisha kivuko kukosa nguvu kisha kuzama.

 
Kivuko cha Mv Kilombero kikiwa kimezama.

Kufuatia ajali hiyo viongozi mbalimbali walifika akiwemo waziri wa ujenzi mawasiliano na uchukuzi Profesa Makame Mbarawa ambapo amsema tukio hilo nikubwa na kuagiza vikosi vya uokoaji kufika mara moja ili kuanza zoezi hilo ikiwa na pamoja na kurudisha mawasiliano ya haraka kwa wananchi hao.

Aidha waziri Mbarawa amesema ipo haja ya kutafuta suluhisho la tatizo hilo ambapo amesema serikali imetenga shilingi milioni 885 kwa ajili ya kumalizia mradi wa daraja hilo ili kuondoa kero kwa wananchi wa wilaya za Kilombero na Ulanga huku akiwataka wananchi kuwa na utulivu wakati serikali ikiendelea kushughulikia tatizo hilo.

Source: ITV

0 comments:

Post a Comment