6 Dec 2015

WALIO RUHUSU USAFIRISHAJI WA MAGOGO NCHINI WATIWA MBARONI, SOMA HAPA MKASA MZIMA.


Shehena ya magogo yaliyo ingizwa nchini kinyume na sheria.

Mkuu wa mkoa wa Rukwa Bw Magalula Said Magalula, ameamuru kukamatwa afisa forodha wa kituo cha Kasesya mpakani na nchi ya Zambia Michael Mwingira, baada ya kuruhusu kuingia nchini shehena ya magogo kutoka nchi hiyo ya jirani, licha ya kujua kuwa mzigo huo uliokuwa umewekwa kwenye kontena kubwa kwa ajili ya kupelekwa nchini China, ulikuwa umejaa utata mkubwa.

Mkuu wa mkoa huyo Bw Magalula Said Magalula akiongea katika kijiji cha Kasesya kwenye mpaka wa nchi ya Zambia wilayani Kalambo, baada ya kukagua kontena hilo la futi 40 lililokuwa na shehena ya magogo zaidi ya 300 ya mti wa Mkurungu, uliopigwa marufuku kuvunwa hapa nchini, amesema anashangazwa kuona mzigo huo ambao una vibali vilivyojaa utata mkubwa, na ambao ulipaswa kupitia nakonde nchini Zambia na kuingilia Tunduma umepitishwa kituo cha Kasesya ukielekea nchini China.

Akiongea mpakani hapo meneja wa kanda wa mamlaka ya huduma za misitu nchini ya TFS Bw Bruno Mallya, amesema nchi za Zambia na Tanzania zimepiga marufuku kwa pamoja usafirishaji wa magogo, kwa lengo la kulinda misitu iliyoharibiwa kwa kiasi kikubwa mno, huku mkuu wa wilaya ya Kalambo Bw Williamana Ndile akisema kuwa kumekuwepo na mchezo mchafu unaofanywa na baadhi ya watu wasiokuwa waaminifu, wa kuvuna miti hiyo ya Mkurungu nchini na kuivusha kwa magendo upande wa pili nchini Zambia.

Katika hali ya kushangaza afisa forodha wa mkoa wa Rukwa Bw Marko Nyamanga, akitetea juu ya upitishaji wa shehena hiyo ya magogo kwenye kituo hicho cha Kasesya, amesema wanafanya hivyo licha ya upande wa pili wa Zambia kutokuwa na mfumo (system) wa upatikanaji wa taarifa za mizigo, hali inayotia shaka kubwa.

 Source: ITV TANZANIA

0 comments:

Post a Comment