16 Dec 2015
KWA SHERIA HII YA KULIPWA KWA KILA NYIMBO ZIKICHEZWA KWENYE TV NA RADIO, WASANII MME HULA, SOMA HAPA.
By Unknown at 15:10
No comments
Nikki wa pili na Joh Makini, (Picha kutoka makitaba).
Akiongea na ripota wa millardayo.com alisema’Leo kulifanyika mkutano mdogo ambapo mawaziri wawili (Waziri wa Viwanda na Biashara & Waziri wa Utamaduni/Sanaa na Michezo cha msingi ilikuwa ni kwamba imezinduliwa rasmi sheria ile imepitishwa ya kulipwa mirabaa ambapo kazi za wasanii zinapokuwa zinachezwa kwenye Ma Redio na TV wanatakiwa walipwe’ -Nikki wa pili
‘Sheria hiyo imesainiwa rasmi kwahiyo kuanzia tarehe 1 January 2016 nyimbo ambazo zitakuwa zinachezwa kwenye TV na Radio zitakuwa zinalipiwa na sio kila TV na au kila Redio zitakua zinalipa sawa hapana utalipa kulingana na mapato unayopata’ Nikki wa pili
‘Kwa hiyo mirabaa itakuwa inakusanywa na Cosota sio wasanii watakuwa wanachukua,Cosota ndio itakuwa inahusika kuchukua na kuwalipa wasanii’- Nikki wa pili
‘Na CMEA kazi yao ni kuhakikisha zile takwimu Cosota halafu Cosota kupitia zile takwimu ambazo zimewasilishwa watakusanya hiyo mirabaa kwenye TV na Radio halafu wao sasa ndio watahusika kuwalipa wasanii’ – Nikki wa pili
Waziri Nape nnauye.
Source: Millardayo.com
0 comments:
Post a Comment