24 Sept 2015

KAMA KIJANA JIFUNZE HAYA KUTOKA KWA MFANYABIASHARA, MJASIRIAMALI MOHAMED DEWJI.

Kijana wa Tanzania Mfanyabiashara mjasiriamali maarufu na aliyekuwa mbunge wa singida mjini bwana  Mohammed Dewji, amejinyakulia tuzo ya kiongozi wakibiashara wa mwaka iliyotolewa huko nchini  Marekani.


Bwana Mohammed Dewji

Kijana uyo anaye miliki kampuni iitwayo Mohammed Enterprises inayohusika na maswala ya biashara za usafiri, chakula, mavazi na kilimo ameonesha mafanikio na uwezo mkubwa katika biashara zake kiasi cha kuingia katika orodha ya matajiri, mabilionea 29  akiwa tajiri kijana kuliko wote barani Afrika ambapo jarida la Forbes la Marekani lilimtaja Mr Dewji kumiliki dola za Marekani billion 1.3( sawa na Tsh trilioni 2.34) ambazo zimetokana na biashara mbalimbali anazozifanya katika kampuni hiyo.


Baadhi ya bidhaa za kampuni ya Mohammed Enterprises.

Akihojiwa na mtangazaji wa bbc swahili, bwana Dewji amesema siri ya mafanikio yake ni kuhangaika, ameheleza kua huwa anaamka saa 12 asubuhi nakwenda miangaikoni mpaka saa 2 au 3 usiku, pia kingine kilichochangia mafanikio hayo ni kuanza biashara akiwa kijana mdogo.
Pamoja na yote aliyoeleza bwana Dewji, kama kijana wa tanzania kuna mengi ya kujifunza ikiwemo kufanya kazi bila kukata tamaa bila kujali aina ya biashara unayofanya alimradi kwa kiasi fulani inamasoko na inakupatia kipato flani( kuhangaika).
Kitu kingine tunachotakiwa kujifunza kama kijana kutoka kwa mfanyabiashara huyu ni kuanza mipango na matimizo ya biashara mapema bila kusubiri mpaka uwe mtu mzima, (kuanza biashara akiawa kijana mdogo).


Mohammed's Quote.

0 comments:

Post a Comment