24 Sept 2015

TAMKO LA TFF JUU YA USHABIKI WA KISIASA KATIKA MECHI YA SIMBA NA YANGA JUMAMOSI.

Wakati tukisubili kwa hamu pambano la watani wa jadi timu za Simba na Yanga, linalotegemea kufanyika tarehe 26 mwezi huu wa 9, Shirikisho la soka Tanzania (TFF) limeonya mashabiki wa pande zote mbili juu ya kutojihusisha na vitendo vyovyote vyenye kurenga ushabiki wowote wa kisiasa hasa siku ya pambano hilo.

Logo za Simba na Yanga

Ofisa wa habari TFF, Baraka Kizunguto amesema kua shirikisho hilo halifungamani na upande wowote wa siasa, dini, kabila wala rangi hivyo halito sita kuchukua hatua kwa yeyote atakae onekana kujihusisha na maswala hayo na kuwashauli mashabiki kutokuja vitu vyovyote vinavyo hashilia siasa.


Pia TFF imetangaza wazi viingilio vya siku hiyo ya pambano ambapo mchanganuo nikama hifuatavywo hapa chini;

  • Tiketi kwahajili ya jukwaa la VIP (A) ni Tsh 30,000/=
  •  Tiketi kwahajili ya jukwaa la VIP(B) ni Tsh 20,000/=
  • Tiketi kwahajili ya jukwaa zilizo bakia kwa Tsh 7000/=
Pambano hilo linalo tegemea kua la kukata na shoka litafanyika katika uwanja wa Taifa Dar  es salaam hipatapo saa kumi kamili jioni.

Uwanja wa Taifa ambamo pambano la Simba na Yanga linategemewa kufanyika.

0 comments:

Post a Comment