5 Aug 2016

WATAALAMU MUHIMBILI WATAJA AINA TANO ZA VYAKULA HATARISHI KIAFYA, ZI CHEKI HAPA.



Afya za wananchi mbalimbali zipo hatarini, kutokana na ulaji wa vyakula mbalimbali ambavyo ni hatari kiafya. Wataalamu wa chakula na lishe wameainisha aina tano za vyakula ambavyo ni hatari katika mwili wa mwanadamu, vikitajwa kusababisha maradhi mbalimbali.

Kwa mujibu wa wataalamu hao, walaji wa nyama ya nundu ya ng’ombe, ngozi ya kuku, clips na bisi wapo katika hatari kubwa ya kupatwa na magonjwa yasiyokuwa ya kuambukiza ikiwamo shinikizo la damu na ugonjwa wa moyo.

Taarifa hiyo inakuja baada ya mtaalamu wa lishe ya Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Ulumbi Kilimba kulieleza gazeti la Mtanzania kuhusu athari za ulaji wa chips.

Akizungumza, Afisa Lishe wa Taasisi ya chakula na Lishe Tanzania (TFNC), Julieth Shine, alisema si chips pekee ambazo ni hatari bali vyakula ambavyo hukaangwa kwa kutumbukizwa kwenye mafuta ni hatari kiafya.

CHANZO: GAZETI LA MTANZANIA

0 comments:

Post a Comment