15 Aug 2016

HAYA NDIO ALIYOYASEMA MGOSI WA SIMBA BAADA YA KUSTAAFU SOKA.

Mgosi akiwaaga mashabiki wa Simba 

Siku ya Jumapili ya August 14 2016 ilikuwa ni siku ya kihistoria kwa mashabiki wa Simba na nahodha wa klabu hiyo Musa Hassan Mgosi ambaye ndio siku aliyotangaza rasmi kuachana na soka la ushindani na kuwa meneja wa timu ya Simba, Mgosi alicheza mchezo wa mwisho na kuagwa kwa heshima na viongozi na mashabiki wa soka.
Mgosi alipo hojiwa alisema hv “Katika kazi ya mpira kuna mambo mengi, nashukuru Mungu hadi namaliza mpira sijapata majeraha yoyote makubwa, kilichonifanya nistaafu nimefikiria kikubwa nilichotakiwa kufanya Simba nimemaliza na hakuna kingine zaidi ya kuhamasisha vijana, leo hii siwezi tena kugombania namba na Ajibu au mwingine huu ni wakati wao”
Hili kusikia mengi zaidi aliyosema, cheki video hapa chini.....


Source: Millardayo.com

0 comments:

Post a Comment