1 Nov 2015

MABOMU YA KUTEGWA YALIPUKA YENYEWE ZANZIBAR NA KULETA HOFU KUBWA KWA WANANCHI, HABARI KAMILI HAPA.


Picha ya Mfano wa bomu, kutoka maktaba.

MABOMU mawili yanayosadikiwa kuwa yalitegwa na watu wasiojulikana, yamelipuka yenyewe na kuzua taharuki kubwa katika eneo la Michenzani mjini Zanzibar.
Kamanda wa Kikosi cha Operesheni na Mafunzo cha Jeshi la Polisi Zanzibar, Juma Yussuf alithibitisha jana kulipuka kwa mabomu hayo, alisema uchunguzi zaidi unaendelea, kujua wahusika wa matukio hayo.
Juzi askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), walifanikiwa kutegua bomu moja, lililotengwa karibu na Kituo cha Polisi cha Darajani bila ya kusababisha madhara.
Matukio hayo, mawili yamezua hofu na wasiwasi kuhusu amani na usalama wa wananchi wa Zanzibar.

0 comments:

Post a Comment