4 Oct 2015

TANZIA: MCHUNGAJI CHRISTOPHER MTIKILA AFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA GARI.

Mwanasiasa mashuhuri nchini Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Democratic Party (DP), Mchungaji Christopher Mtikila amefariki dunia na watu wengine watatu kujeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea katika Kijiji cha Msolwa kilichopo Chalinze mkoani Pwani alfajiri ya leo tarehe 04/10/2015.
mtikila
Picha zikionesha ajari ya gari iliyo sababisha kifo cha Mchungaji Mtikila.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Jafari Mohamed, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa "Taarifa za mwanzo" zinasema Mtikila amefariki majira ya saa 11:45 alfajiri ya leo katika kijiji cha Msolwa, Chalinze, amesema gari alilokua amepanda Mchungaji Mtikila lilikua linatoka mkoani Morogoro kwenda jijini Dar es salaamu, ndani ya gari hilo kulikua kuna watu wanne ambapo wamepatikana majeruhi watatu ambao walikimbizwa katika hosiptali ya Tumbi iliyopo Kibaha Pwani kwa matibabu.
Mchungaji Christopher Mtikila enzi za uhai wake.
Uongozi wa blog ya kijana huru inatoa pole kwa familia yote iliyofikwa na msiba kwani inatambua mchango wa Mchungaji Mtikila katika kukuza siasa na kusimamia demokrasia katika nchi yetu hii ya Tanzania, Mungu alitoa naye ametwaa jina lake libarikiwe.
Source:global publishers

0 comments:

Post a Comment