2 Oct 2015

LAITI UNGEJUA JINSI NGONO ILIVYO NA NGUVU USINGE THUBUTU KUFANYA NA MTU YEYOTE,SOMA HAPA UELEWE USIJE UKALAUMU HUKUAMBIWA.



Wakati wa kujamiiana kuna mabadilishano tofauti tofauti  kati ya pande mbili yanayotokea kimwili na kiroho (yani kati ya mwanaume na mwanamke). Watu wengi wanafahamu mabadilishano ya kimwili tu (physical exchange of emotions). Lakini ukweli ni kwamba kunamabadilishano ya kiroho pia ambayo watu wengi hawajui, Wakati unafanya ngono na mtu kunakuwepo na ubadilishano wa kiroho (spiritual exchange) kama vile kuchukua sifa, tabia, itikadi, mwenendo, mikosi na bahati mbaya au nzuri (ikiwemo umasikini ama utajiri) ya uyo unaye fanyanae ngono kwa sababu unapofanya ngono unakuwa sehemu ya mwili wake. Ngono iliumbwa na Mungu mwenyewe maalumu kwa mwanaume mmoja na mwanamke mmoja (yani mume na mke) kwa lengo la kuzaliana na kujaza dunia, hivyo matatizo mengi huja kutokana na kufanya ngono kabla au nje ya ndoa.
Unapofanya ngono na mtu (pengine asiye mke au mume wako) unaingia katika agano la kiroho naye pamoja na kwamba kimwili utaona burudani lakini kiroho si kawaida na matokeo yake unahishi kwa kufuata masharti  na taratibu za hizo roho ulizoingianazo maagano. 
Jinsi ya kuepuka haya ni kuacha kufanya ngono isiyo sahii (ngono kabla ya ndoa) kuanza kufuata njia ya Mungu(kusali sana) na kusubiri mtu sahii kwa muda sahii ambao ni muda wa ndoa, epuka kutazama picha za jinsia nyingine hovyo zikiwa na nguo au zisipokua na nguo(pornography) pia epuka kutengeneza hisia(mawazoni) za kua unafanya ngono na mtu flani (hii hasa kwa wavulana), muda mwingine utumie kwa kufanya mazoezi, na kujishugulisha na shughuli nyingine zitakazo kufanya uwe bize, na unapokua huru basi jaribu kujumuika na wenzako na muzungumze mambo sahii, pia kama utabahatika kuwa na mwezi wako katika kipindi chote cha urafiki na uchumba muheshimiane, na kuwa na nidhamu ya kusubiriana kwa kutofanya ngono mpaka muda sahii ufike.MUNGU ATUSAIDIE SOTE HASA VIJANA.

0 comments:

Post a Comment