29 Sept 2015

WANANCHI WA KAGERA WALILIA MAKANISA YAO YALIYO CHOMWA MOTO, TAZAMA NAMNA YALIVYO HARIBIWA.

WaTanzania ni watu tunaopenda amani na tuna uhuru wa kuchagua imani bila kujali lugha, kabila wala rangi , na tumeweza kutunza amani hii toka Tanzania yetu iundwe, lakini katika hali isiyo ya kawaida uko bukoba mkoani kagera kumetokea matukio ya uchomaji wa makanisa uliofanywa na watu wasiojulikana.

Moja kati ya vifaa vya kanisa vilivyoteketezwa.

Makanisa yaliyo chomwa ni ya Pentecostal Assemblies of God (PAG) eneo la Buyekera, Living
Water Internationa na Evangelical Assemblies of God (EAGT) kata ya Kibeta huko wilayani Bukoba baada ya matukio hayo ya uchomaji wa makanisa siku mbili badae imetokea tena tukio la watu wasiojulikana kubomoa makufuli ya Makanisa na kufanya huaribifu ndani ya makanisa hayo, jambo linalopelekea kuwakosesha raha wahumini, wananchi wa Kagera na WaTanzania kwa ujumla.
Wachungaji hasa wa makanisa hayo yaliyo haribiwa wametoa masikitiko yao na wamewataka polisi kushughulikia maswala hayo ikiwemo kuwatafuta na kuwashughulikia wahusiaka.

Moja ya kanisa lililo chomwa vibaya.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Kagera, bwana Augustine Oromi, amethibitisha kutokea kwa matukio hayo.
8
Moja kati ya viongozi wa makanisa yaliyo haribiwa uko bukoba akizungumza kwa uchungu.

0 comments:

Post a Comment