Hugh Grosvenor anafanya kazi katika kampuni ya Bio-bean, kampuni inayoangazia teknolojia isiyoongeza gesi zinazochangia ongezeko la joto duniani.
2 na 3. Alexandra Andresen na Katharina Andresen
Alexandra mwenye miaka 20 na Katharina mwenye miaka 21 ndio wachanga zaidi na wanamiliki kampuni ya Ferd, binti hawa walirithi utajiri hu kutoka kwa baba yao Johan, raia wa Norway mwaka 2007.
4. Gustav Magnar Witzoe
Ni kijana mwenye miaka 23, anatokea Norway, amerithi sehemu ya biashara ya babake ya kufuga samaki na sasa utajiri wake ni $1.1bn (£846m).
Gustav Witzoe, baba yake ambaye wana jina sawa, alimpa hisa kwenye kampuni hiyo kama zawadi lakini hana udhibiti au usemi wowote.
5 na 6. Ludwig Theodor Braun na Eva Maria Braun
Familia yao ilianzisha kampuni ya dawa ya B. Braun Melsungen, Ujerumani mnamo mwaka 1839.
Kampuni hiyo ni maarufu sana kwa dawa na vifaa vya matibabu.
Ludwig humiliki 10% ya kampuni hiyo ambayo ni sawa na $1.8bn (£1.4bn) na dada yake Eva Maria Braun yuko nyuma yake kidogo lakini utajiri wake ni $1.4bn (£1bn).
7 na 8. Evan Spiegel na Bobby Murphy
Ni kati ya waanzilishi wa mtandao wa Snapchat ambao hutumiwa na mamilioni ya vijana duniani.
Evan Spiegel ana umri wa miaka 26 na utajiri wake ni $2.1bn (£1.6bn) na Bobby Murphy mwenye miaka 28 na utajiri wake ni $1.8bn (£1.3bn).
9. Lukas walton
Lukas Walton mwenye miaka 29, anatoka katika familia tajiri inayomiliki Walmart (miongoni mwa kampuni nyingine), ambayo pia humiliki Asda nchini Uingereza, Utajiri wake ni $10.4bn, ambazo ni karibu £7.2bn kwa viwango vya sasa vya ubadilishanaji wa fedha.
10.Wang Han
Ni raia wa China, Chanzo cha utajiri wake ni urithi wa hisa za kampuni ya ndege ya Juneyao Air kutoka kwa baba yake Wang Junyao aliyefariki 2004.
Junyao alikuwa mwanzilishi wa kampuni ya Juneyao Group. Wang Han humiliki 27% ya hisa za shirika hilo la ndege na 14% ya hisa za maduka ya jumla ya Wuxi Commercial Mansion Grand Orient, Utajiri wake unakadiriwa kuwa $1.34bn.
0 comments:
Post a Comment