Lakini katika mchezo wamarudio kati yao na Mobejaia ya Algeria, Yanga imeonesha kufufua matumaini membamba baada ya kucheza mchezo safi na mzuri huku wakiibuka vifua mbele kwakuongoza kwa gori moja lililofungwa na Amisi Tambwe, katika mchezo uliopita Yanga ilifungwa bao moja na timu hii ya Mobejaia mchezo uliochezwa huko Algeria.
Miamba hiyo ya Tanzania imecheza mchezo huo wa marudio huku ikimkosa mchezaji wake Dornald Ngoma aliekua na kadi mbili za njano.
Kwa mchezo huu waliouonesha Yanga leo ni dhahiri kua Timu ya Mobejaia watarudi kwao na kusimulia kilicho wapata.
Kwamchezo huu waleo Yanga sasa itakua na pointi 4 huku ikiendelea kushikilia mkia ambapo timu inayo ongoza kwa pointi nyingi ni TP Mazembe yenye point 10 ikifuatiwa na Mobejaia na Medeama zenye pointi 5 zote.
Kama waTanzania tunawatakia kilaraheli Miamba hii ya Tanzania Young Africans ama Yanga katika mashindano ayo.
0 comments:
Post a Comment