12 Aug 2016

HUU NDIO UKWELI NA UFAFANUZI JUU YA TIMU YA YANGA KUKODISHWA NA MANJI KWA MIAKA 10.

Baadhi ya wachezaji wa Timu ya YANGA wakishangilia gori
Zile fununu kuhusiana na klabu ya Dar es Salaam Young Africans (YANGA) kutaka kukodiwa na mfanyabiashara na mwenyekiti wa klabu hiyo Yusuph Manji, kuna baadhi ya watu ambao wamekuwa wakipokea taarifa tofauti kuwa klabu hiyo tayari mwenyekiti wao Manji kakodishwa kwa kipindi cha miaka 10.
Mwenyekiti wa timu ya YANGA bwana Manji
kaimu katibu mkuu wa Yanga Baraka Deusdedit alitafutwa ili aweke wazi kuhusiana na suala hilo, kuhusu je ni  kweli Yanga imekodishwa au bado?
Akiongea, bwana Baraka Deusdedit  alisema “Kiukweli bado haijakodishwa bali mwenyekiti alikuja na wazo hilo na kapeleka kwa bodi ya wadhamini ndio wanamamlaka ya kuzungumzia hilo, lakini kuhusu taarifa zinazosambazwa kuwa tayari imekodishwa sio kweli kwani mikataba ikiwa tayari wanachama watapewa fursa ya kuiona na kutoa mawazo yao”
Msikilize hapa chini kwenye video hii akielezea zaidi...

CHANZO: Video toka Millardayo.com

0 comments:

Post a Comment