23 May 2016
HII NDIO NDEGE ILIYO TENGENEZWA KWA AJILI YA MATUMIZI YA NYUMBANI, ITAZAME HAPA
Nchini Ujerumani wametengeneza Ndege aina ya LILIUM kwa ajili ya matumizi ya nyumbani yenye siti mbili, shepu ya yai na inatumia umeme, imetengenezwa na mainjinia wanne wakijerumani wakidai kuwa ndege hiyo yenye kupunguza matumizi na kurahisisha usafiri kwa watu.
Ndege hii inasemekana kuwa na uwezo wa kwenda hadi spidi ya kilometa 400 kwa saa, kutumika kwenye eneo tambarare, kupaa na kutua kwa mita 15. Kingine kikubwa ni kwamba inatumia umeme na inachajiwa kama simu pia haina kelele pia ni kwa ajili matumizi ya mchana tu kwenye hali ya hewa tulivu na sio usiku.
Mmoja wa msaidizi wa mmiliki wa ndege hiyo, Daniel weigand amesema wana mpango wa kuiingiza sokoni mwaka 2018, ameyazungumza haya …
”tunataka ndege isiyo na gharama kubwa wala isiyokuwa na tatizo la utumiaji wa miundombinu yake, pia iweze kutumika na watu wengi wenye uwezo wowote ule sio watu wenye uwezo mkubwa tu ndo waweze kununua ndege hii”.
Source: millardayo.com
0 comments:
Post a Comment