23 May 2016

HII NDO KAULI YA TCRA KUHUSU MUDA WA KUZIMWA SIMU FEKI


Meneja mawasiliano wa mamlaka ya mawasiliano Tanzania Innocent Mungi amesema muda wa kuzima simu bandia hautabadilishwa wala kusogezwa mbele na kuwataka wauzaji na wanunuzi wake kuwa makini ili kutojiingiza katika matatizo.

Meneja mawasiliano wa mamlaka ya mawasiliano Tanzania Innocent Mungi

Mungi ameyasema hayo alipokuwa akiongea na wauzaji na watumiaji wa simu mkoani Geita amesema hakuna mtu yeyote atakayelipwa fidia pindi simu zitakapozima hivyo kuwataka wauzaji kuachana na uagizaji na usambazaji wa bidhaa zisizokuwa na ubora ili kuepukana na madhara mbalimbali yanayoweza kujitokeza.

Naye mkuu wa mkoa wa Geita Meja Jenerali Ezekiel Kyunga ameyataka makampuni ya simu kuhakikisha wanaboresha mawasiliano hasa vijijini kutokana na mahitaji ya muhimu waliyonayo kutokana na changamoto ya miundombinu.

Baadhi ya wafanyabiashara wa simu mkoani Geita wamesema kwa sasa biashara yao imeharibika kutokana na taarifa za kuzimwa na kufungiwa kwa simu bandia na kuomba uongezwe muda kwani mpaka sasa wana mzigo mkubwa ambao bado haujauzwa.

Source: ITV TANZANIA

0 comments:

Post a Comment