13 Dec 2015
KUMBE HIKI NDICHO KIPAJI KINGINE CHA YAYA TOURE UKITOA MPIRA WA MIGUU, KITAZAME HAPA.
By Unknown at 11:20
No comments
Yaya Toure akiwa na jezi ya timu ya Manchester City.
Yaya Toure, mchezaji mpira wa miguu katika klabu ya Manchester City na timu ya Taifa ya Ivory Coast ana kipaji kingine kikubwa cha mchezo wa Karate.
Mchezo wa Karate alianza akiwa bado kijana mdogo kabisa na huenda pengine ndio angeendelea nao mpaka sasa kama asinge katazwa na baba yake mzee Toure maana ulikua ukimletea majeraha ya mara kwa mara.
Akiwa mdogo aliweza kufanya vizuri sana katika mchezo huo wa Karate mpaka kufikia hatua ya kuchaguliwa katika mashindano makubwa yaliyokua yafanyike Kenya lakini hakuweza kuhuzuria kutokana na kukatazwa na baba yake.
Pamoja na yote bado Yaya Toure ana kipaji cha mpira wa miguu na amekua akifanya vizuri sana ambapo ameweza kutunikiwa tuzo ya uchezaji bora afrika inayo tolewa na BBC kila mwaka.
Yaya Toure akiwa ndani ya jezi ya taifa la ivory coast.
0 comments:
Post a Comment