23 Oct 2015

MAHAKAMA KUU TANZANIA YATOA TAMKO KUHUSU UMBALI SAHIHI WA KURINDA KURA, SOMA HAPA KILICHOSEMWA.


Jengo la Mahakama.
Mahakama Kuu Dar imetupilia mbali shauri la tafsiri ya sheria ya mpigakura kukaa au kutokaa umbali wa mitaa 200 kutoka eneo la kupigia kura.
Kwa mujibu wa majaji waliotoa maamuzi hayo wamesema kuwa, kwa kuwa mikutano ilishakatazwa kuwepo siku ya uchaguzi, hivyo hakuna mkutano, mkusanyiko au vikundi vyovyote vitakavyoruhisiwa siku hiyo na kufanya hivyo ni kuvunja sheria.
Pia wameeleza kuwa siku ya uchaguzi mtu yeyote atakayevaa sare ya chama chochote naye atakuwa amevunja sheria.
Kwa upande wa wakili wa utetezi,  Peter Kibatala amesema ameyapokea maamuzi hayo lakini atakata rufaa juu ya shauri hilo kwa manufaa ya chaguzi nyingine zijazo.


Mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Ernest Mangu.
Nalo Jeshi la Polisi limewataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika zoezi la kupiga kura kwani ulinzi utakuwa umeimarishwa vya kutosha na kuongeza kuwa siku hiyo likitokea kundi lolote linalowatishia watu kwenda kupiga kura watalichukulia hatua za kisheria.
Hayo yamesemwa na mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Ernest Mangu wakati wa kuhitimisha kongamano lilowahusisha viongozi wa dini, wanasiasa na wakuu wa mashirika mbalimbali ya kimataifa uliokuwa na lengo la kujadili amani hapa nchini.

0 comments:

Post a Comment