29 Oct 2015

KIMENUKA!!! MGOMBEA MWENZA WA LOWASSA, JUMA DUNI HAJI APELEKA PINGAMIZI NEC ZIDI YA MATOKEO YA URAISI YANAYOENDELEA KUTANGAZWA.


Juma Duni Haji akiwa amazongwa na waandishi wa habari katika ukumbi wa Mwl Julius Nyerere.

Mgombea mwenza wa kiti cha  uraisi  wa Edward Ngoyai Lowassa kupitia UKAWA , Juma Duni Haji amezuiwa kuingia katika chumba cha kutangazia matokeo ya urais katika ukumbi wa Julius Nyerere wakati zoezi hilo likiendelea baada ya kueleza kuwa ameleta hati ya pingamizi ya matokeo.
Hata hivyo walinzi wa eneo la kutangazia matokeo walimkatalia kuingia katika chumba hicho na kumtaka aende Makao Makuu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuwasilisha hati yake hiyo na kisha kusindikizwa kwenye gari alilokuja nalo lenye namba T754 DDY aina ya Toyota.

0 comments:

Post a Comment