4 Oct 2015

HILI NDILO TAMKO KUTOKA TANESCO LINALO ELEZA SABABU ZA MGAO WA UMEME KUENDELEA LICHA YA MITAMBO KAZAA YA UZALISHAJI UMEME KUWASHWA.




Shirika la umeme Tanzania, TANESCO limesema kua mgao wa umeme unao endelea nchini unasababishwa na kushuka kwa uzalishaji wa umeme katika mabwawa ya maji kwa asilimia 81.3.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi mtendaji wa TANESCO Mhandisi Felchesmi Mramba, amesema uwezo wa juu wa mitambo ya uzalishaji umeme kwa kutumia maji ni megawati 561 ambapo kwasasa mitambo hiyo inazalisha megawati 105 tu ambazo ni sawa na asilimia 17.3.

Mkurugenzi mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Felchesmi Mramba.

Akizungumzia kuhusu umeme unaozalishwa kwa njia ya gesi na kampuni ya Pan African amesema nao umeshuka kutoka megawati 340 hadi kufikia megawati 260 tu.
Ameelezea pia kua ile mitambo ya kuzalisha umeme kwa gesi ya bomba jipya iliyo washwa hivi karibuni inazalisha megawati 190 na wanatarajia kuongeza nguvu nyingine ya umeme ya megawati 35. Alisema mwezi wa 9 waliwasha mtambo uliozalisha umeme wa megawati 20 kutoka bomba la gesi la songosongo na kuongeza umeme kwa jumla ya megawati 110.
Alisema uwezo wa uzalishaji wa umeme kwa mitambo ya mafuta ni megawati 230 lakini kwasasa inazalisha megawati 190 tu.

Mitambo ya kupokelea gesi asilia eneo la Kinyerezi.

Shirika hilo la umeme limesema mitambo mingine ya Symbion (megawati 20),Ubungo II (megawati 35), Songas (megawati 20) na Kinyerezi (megawati 70) inatarajia kuwashwa ndani ya wiki moja hadi mbili tangu sasa ili kukabiriana na tatizo hilo la mgao.

Source:mwananchi

0 comments:

Post a Comment