23 Aug 2016

UFAFANUZI WA WAZIRI WA AFYA JUU YA KAULI YA RAISI MAGUFULI KUHUSU KUFYATUA WATOTO.

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema kauli ya Rais kwa Watu Dar kuwa "wafyatuwe" tu watoto maana eleimu itakuwa bure ilikuwa ni utani tu kwa Wazaramo,kwa sababu sera ya Taifa mpaka sasa ni uzazi wa mpango.
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu
Kauli hiyo ameitoa alipokuwa anaongea na waandishi wa Habari kuweka sawa kauli hiyo ya Rais. Ummy Mwalimu anasema baada ya kauli hiyo kumekuwa na mijadala na kauli za kukinzana na Sera ya Taifa ya Uzazi wa Mpango,Lishe bora na Afya kwa watoto.Mh.Ummy anasema kauli ile isichukuliwe kama ni sera ya Taifa kwa sasa na wala siyo kauli "serious" bali ni utani wa Rais kwa watani zake Wazaramo,na ndio maana Rais alisema "Watani zangu Wazaramo".

Msimamo wa Wizara ya Afya na Serikali kwa ujumla ni sera ya Uzazi wa Mpango ili kuweza kukabliana na ongezeko la Watu Duniani linaloendana na ukuwaji wa uchumi na maendeleo ya watu.Hivyo Watanzania wanahimizwa kuzaa kwa mpango ili kuweza kumudu familia na kuepuka madhara ya uzazi usio na mpango wa "kufyatuwa" watoto.
Cheki video hapa chini kuona alichosema zaidi...

0 comments:

Post a Comment