23 Aug 2016

KOCHA MKUU WA YANGA ATOA MAPUNGUFU YA UWANJA WA UHURU BAADA YA UKARABATI, CHEKI HAPA.

Kocha mkuu wa Yanga bwana Pluijm
Wakati serikali ikizindua rasimi uwanja wa uhuru baada ya ukarabati, Kocha mkuu wa timu ya Yanga bwana Pluijm amefunguka mapunguvu ya uwanja huo.
Pluijm amesema kua amegundua kwamba katika kapeti la nyasi vipira vya nyasi bandia vitaleta hatari kubwa kwa wachezaji watakaotumia uwanja huo itakayo sababisha majeruhi kuongezeka.

                                                             Uwanja wa uhuru
Amesema janvi hilo la nyasi bandia limekua gumu kiasi cha kuzuia mpira kudunda vizuri na kwa ugumu huo litaleta usumbufu kwa wachezaji ikiwemo ongezeko la majeruhi, alongeza kua uwanja huo umekua kama uwanja wa mchangani kwani nyasi hizo zilitakiwa ziwe laini kama zile za uwanja wa karume na vingine viwili vya zanzibar na kwa ugumu huo zitawaumiza wachezaji.
Baadhi ya nyasi bandia katika uwanja wa uhuru
Pluijm ambaye timu yake ya Yanga ilifanya mazoezi mara mbili katika uwanja huo kabla ya kwenda congo kupambana na timu ya TP Mazembe katika kukamilisha ratiba ya kombe la shirikisho Afrika ambapo Yanga ndio timu yenye point ndogo zaidi ya timu zote shiliki.

Chanzo: Mwanaspoti

0 comments:

Post a Comment