26 Aug 2016

CHEKI HAPA PICHA NA KINACHOENDELEA KWENYE TUKIO LA MAJAMBAZI UKO MKURANGA.



Mapigano makali yalikua yakinaendelea kati ya polisi na watu wanaosadikiwa kuwa majambazi eneo la Vikindu, wilaya ya Mkuranga, mkoa wa Pwani.

Aidha taarifa za awali ziliripoti kuwepo na majibizano ya risasi kati ya jeshi la Polisi na watu hao wanaodaiwa kuwa ni majambazi toka usiku wa kuamkia leo na inadaiwa kuwa askari mmoja ameuawa kwenye mapigano hayo.

Image result for majambazi mkuranga

Majambazi ambao idadi yao haijajulikana wanadaiwa kuuwawa katika mapigano hayo  kati yao na polisi, Milio ya risasi na mabomu viliendelea kusikika kunzia saa saba usiku kuamkia leo katika eneo hilo ambalo majambazi hao walikuwa wamejificha.

Hatimaye milio ya risasi haisikiki tena eneo la tukio na wanachi wameambiwa wasisogelee eneo hilo.

Taarifa inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii ambayo hatujaweza kuithibitisha mara moja inasomeka hivi; “Majambazi 14 wameuawa na majambazi 5 wamekamatwa wakiwa hai mmoja wa majambazi waliokamatwa wakiwa hai ni Kanali mstaafu ambaye ni sniper (mlenga shabaha).  Alikuwa mwanajeshi, na alipata mafunzo ya ujasusi na kulenga shabaha kwa miaka 3 huko nchini Cuba kabla ya mafunzo yake kukatishwa baada ya kubainika kuwa sio RAIA.”
“Tumempotezakamanda Mwandamizi wa Kikosi cha Kuzuia Ujambazi. Tunamuombea alale pema peponi.  Amefanyakazi nzuri ingawa imechukua uhai wake ila ametutetea na kutuacha tukiwa hai.”


0 comments:

Post a Comment