Caster Semenya
Jambo la kwanza
Mwaka 2008 baada ya kushinda mbio za dunia ,wanariadha wenzake wa kike walilalamikia umbile lake mmoja akimwita haswa mwanamume.
Jambo la pili
Mwaka 2009 alipigwa marufuku kushiriki kwenye riadha ,Shirika kuu la Riadha duniani IAAF lililazimika kumfanyia uchunguzi wa kubaini jinsia yake baada ya umbile lake kubadilika na kufanana na la kiume.
Uchunguzi wa madaktari ulibaini kuwa alikuwa mwanamke lakini alikua na homoni za kimapenzi za kiume yaani hyperandrogenism, inayosababisha ongezeko la viwango vya testosterone .
Semenya alisikitishwa sana na uchunguzi huo.Alisema kama ingekua sio familia yake kumjali na kumpa mapenzi asingeweza kuvumilia uchungu alioupata akisema ni kama alidhalilishwa kwa watu wote duniani kuhusu jinsia yake.
Jambo la tatu
Mwaka 2011 IAAF ilibadilisha sheria ya viwango vya homoni za miume kwa wanawake na kumruhusu Semenya kushiriki,alipoidhinishwa Semenya alinyakuwa fedha kwenye mashindano ya dunia mwaka 2012.
Jambo la nne
Mbali na riadha Semenya anasoma somo la sayansi ya michezo katika chuo kikuu cha Pretoria Afrika Kusini.
Jambo la tano
Mwaka 2015 Semenya alimuoa msichana mrembo kwa jina LedileViolet wa Afrika Kusini.
Jambo la sita
Kwenya mashindano ya fainali ya mita 800 yakinadada Olimpiki siku ya jumamosi shirika la kimataifa la usalama liliweka usalama wa ziada kumlinda Semeya kutokana na mashabiki wa wapinzani kumkashifu kuwa hakufaa kushiriki kwenye mbio za kinadada.
Afrika Kusini inampenda nsana na viongozi kadhaa wamempongeza kwa kushinda dhahabu.
Cheki pia picha mbalimbali za dada Semenya hapa chini,,,,
0 comments:
Post a Comment