10 Aug 2016

PICHA YA YESU AKITOA DAMU MSALABANI YAONEKANA KANISANI NIGERIA, CHEKI HAPA.

2
Kanisa Katoliki la Mtakatifu Agustino ambapo muujiza huo unadaiwa kutokea

Maelfu ya wakazi wa Jimbo la Benue nchini Nigeria, wakristu na wasio wakristu walifurika katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Agustino lililopo karibu na Mji wa Makurdi kushuhudia muujiza wa kuonekana kwa picha ya Yesu msalaani ikitoka damu.
3
Waumini wakiwa wamekusanyika eneo la picha ya Yesu msalabani iliyokuwa ikitokwa damu

Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wanasema waliona picha ya Yesu katika ukuta ndani ya kanisa hilo wakati mashuhuda wengine wakisema waliona picha ya Yesu msalabani ikitokwa damu ambayo ilikuwa ikichuruzika kuelekea miguuni.
Mmoja wa waumini wa kanisa hilo alisema picha ya kwanza ilitokea Ijumaa iliyopita na baada ya taarifa kusambaa sana siku ya Jumapili, kesho yake Jumatatu  wananchi wakakimbilia kanisani hapo kushuhudia miujiza hiyo.
Mwanga mkali kanisani baada ya picha ya Yesu kudaiwa kuonekana

Mmoja wa waumini aitwaye, Emmanuel Hembenkaan alisema picha iliyoonekana ukutani iliambatana na mwanga mkali ambao uliangaza ndani ya kanisa zima.
MMH
Picha ya Yesu msalabani inayodaiwa kutokwa damu

CHANZO:NaijaGists.com
KK: Globalpublishers.com

0 comments:

Post a Comment