Nikijana kama wewe ama pengine ni mdogo kuliko wewe na kama kakuzidi basi ni mwaka mmoja ama miwili, anamika 15 tu, ni mtoto wa pili katika familia ya Mtu mwenye nguvu ya kimadaraka na kifedha duniani.
Anaitwa Sasha Obama, mtoto wa pili wa raisi wa marekani mwenye asili ya kiafrika bwana Barack Obama, ikiwa ni tofauti na desturi ya watoto wengi wanaotoka katika familia tajiri kifedha, binti huyu mrembo anafanya kazi katika mgahawa mdogo tu karibu na bahari ikiwa ni hatua aliyochukua kujitafutia kipato yeye mwenyewe tofauti na kipato kikubwa walichonacho wazazi wake.
Sasa sisi kama vijana tujifunze kitu toka kwa binti huyu, hasa wadada ambao wanajiona wazuri sana kiasi kwamba wanachagua kazi ama wengine kutokufanya kazi kazi kabisa kwakutegemea familia, mpenzi au mme, nasisi wakaka pia lazima tujifunze kitu sio eti kwasababu familia yako ni tajiri basi ubweteke usifanye lolote kuingiza kipato na pia wale wanaojiita wachagua kazi eti kwasababu ni wasomi, mahandsome ama wasafi.
Vijana tubadilike, tujitume tuchangamshe akili kubuni miradi (project) tutafute mitaji tufanye kazi, atakama nikuajiliwa pia nisawa alimradi unapata pesa ya kujimudu, ulimwengu huu wasasa si wakutegemea mzazi,mpenzi, mke ama mme.
TUBADILIKE, USIPOBADILIKA MABADILIKO YATAKUBADILISHA.
0 comments:
Post a Comment