7 Aug 2016

HUU NDIO UKWELI HALISI WA KIFO CHA YULE MWANAFUNZI WA UDOM

picha ya marehemu.....
Fredrick Joseph Kisaina enzi za uhai wake.

kabla ya kukumbwa na mauti, marehemu aliyekuwa akikaa bweni namba tatu chuoni hapo alikuwa akinywa pombe yeye na marafiki zake kwenye baa inayojulikana kwa jina la Carnival iliyopo ndani ya Kitivo cha Sayansi ya Jamii na Lugha.
Kwa mujibu wa chanzo makini, siku ya tukio, saa tano kamili usiku, ulizuka ugomvi baina ya marehemu na watu wengine, hali iliyosababisha wamiliki wa baa hiyo kuwatoa nje kwa maelezo kwamba lile ni eneo la biashara.
Fredrick Joseph Kisaina mwenye chupa ya bia ikiwa ni saa chache kabla ya kufikwa na umauti.

“Kama unavyojua mazingira ya chuo chetu ukitoka pale baa kupandisha huku juu kuna giza, hivyo baada ya kufukuzwa kule baa, walikuja kugombana eneo lenye giza na hapo ndipo marehemu alipochomwa kisu kifuani na kuanguka chini huku akipiga kelele, ambapo walinzi walipofika walimkuta yupo chini huku damu nyingi zikitoka kwenye jeraha,” kilisema chanzo hicho ambacho jina lake linahifadhiwa.

“Walinzi walimpeleka hospitali ambako alipewa huduma ya kwanza na kuwahishwa hospitali ya mkoa ambako ilipotimia saa nane usiku aliaga dunia. Mwili wake ulisafirishwa kwenda kwao kwa ushirikiano wa Jeshi la Polisi mkoani Dodoma na uongozi wa chuo hicho na serikali ya wanafunzi (UDOSO),” kiliongeza chanzo hicho.
Mmoja wa marafiki wa karibu na marehemu aliyejitambulisha kwa jina la Yachi, alisema Fredrick, alikuwa mtu wa ugomvi, aliyependa kutembea na kisu kiunoni.

RAIS WA SERIKALI YA WANAFUNZI KITIVO CHA SANAA NA LUGHA BWANA BRUNO
Rais wa Serikali ya Wanafunzi Kitivo cha Sanaa na Lugha, Bw. Julian Bruno.

Rais wa Serikali ya Wanafunzi, Julian Bruno licha ya kutoa pole kwa wenzake na familia, aliwaasa wanafunzi wenzake kuwa makini katika suala zima la ulevi kwani ni hatari.
Meneja wa baa hiyo aliyejulikana kwa jina la Dada Tatu alipoulizwa kuhusiana na tukio hilo na kama alikuwa anamfahamu marehemu, alifunguka hv “Namfahamu vyema marehemu na nimesikitishwa sana na kifo chake kwa sababu hakuna binadamu anayefurahia kifo cha mwenzake ni vyema wanafunzi wakaachana na ulevi na kuzingatia masomo yao maana ulevi unawapa tamaa, hadi mauti yanamkuta, alishakuwa na matatizo na uongozi wetu,” alisema.
Marehemu Fredrick alizikwa Jumanne kwenye Makaburi ya Nyakato yaliyopo ndani ya Manispaa ya Musoma Mjini, Mkoani Mara.
Mungu alialaze roho yake mahali pema peponi, amina!

CHANZO: global publisher
STORI: Leonard Msigwa, gazeti la Risasi Jumamosi

0 comments:

Post a Comment